25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAKATIBU TAWALA WAPANGULIWA

 

Na NORA DAMIAN, DAR ES SALAAM


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Mkuchika, amefanya uteuzi wa makatibu tawala wa wilaya na kuwahamisha baadhi yao.

Katika uteuzi huo makatibu tawala 18 ni wapya na wanne wamebadilishiwa vituo vya kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, alisema   nafasi hizo zimetokana na sababu mbalimbali zikiwamo kustaafu kazi kwa mujibu wa sheria, kuacha kazi, uhamisho na kupangiwa majukumu mengine kama ya ukuu wa wilaya na usaidizi wa katibu tawala wa mikoa.

Makatibu tawala wapya na vituo vyao vya kazi kwenye mabano ni Stella Msoffe (Kinondoni), Bupe Mwakibete (Temeke), Sheila Lukuba (Ilala), Sara Komba (Mpwapwa), Zahara Michuzi (Chemba), Kodole Kiligala (Bukoba) na Ally Mchome (Mwanga).

Wengine ni Joseph Mabiti (Siha), Michombero Anakleth (Chunya), Kasilda Mgeni (Mtwara), Daniel Zenda (Newala), Petro Sabato (Misungwi), Emmanuel George (Njombe), Charles Mkama (Manyoni), Warda Maulid (Kilindi), Hassan Nyange (Pangani), Boniface Juma (Handeni) na Hamza Athumani (Bagamoyo).

Makatibu tawala waliohamishwa na wilaya walizotoka na wanazokwenda kwenye mabano ni Hashimu Komba (Temeke – Iringa), Edward Mpogolo (Ilala – Dodoma), Ally Nyakia (Chemba – Kondoa) na Yusufu Kasuka (Mwanga – Kigoma).

Waziri  alisema makatibu hao wanatakiwa kuripoti katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora–Dodoma ifikapo Agosti 9, mwaka huu  wakiwa na vyeti vyao halisi vya kumaliza kidato cha nne na sita pamoja na taaluma zao na nakala za vyeti hivyo zilizothibitishwa kwa mujibu wa sheria.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles