24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

RAIS WA VENEZUELA ANUSURIKA KUUAWA

CARCAS,Venezuela


RAIS wa   Venezula Nicolás Maduro, amenusurika kuuawa baada ya  kushambuliwa na ndege isiyokuwa na rubani alipokuwa akihutubia  wakati wa  kuadhimisha miaka 81 ya jeshi la nchi hiyo.

Tukio hilo lilitokea    Caracas jana na katika picha za  video   Rais Maduro anaonyeshwa akitazama juu ghafla kwa hofu huku wanajeshi kadhaa wakikimbia.

Rais  Maduro ambaye alishinda uchaguzi  ulioghubikwa na utata, ameilaumu Colombia kwa shambulio hilo madai ambayo nchi hiyo imeyakanusha.

Taarifa zilisema  katika tukio hilo wanajeshi saba walijeruhiwa na watu kadhaa walikamatwa.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mawasiliano, Jorge Rodriguez, ndege mbili zisizokuwa na rubani   zililipua mabomu karibu na jukwaa la rais.

Rais Maduro baadaye alisema kuwa Kifaa kilichokuwa kinaruka kililipuka karibu  yangu  na sekunde chache baadaye ukatokea mlipuko wa pili.

Picha kwenye mitandao wa jamii zilionyesha walinzi wakimlinda Maduro wakitumia vifaa visivyopenya risasi baada ya shambulio hilo.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,859FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles