25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Makatibu Tawala wa Mikoa waomba elimu ya Anwani za makazi itolewe kwa Watanzania

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

MAKATIBU Tawala wa Mikoa nchini wameomba elimu itolewe zaidi juu ya mfumo wa Anwani ya Makazi Postikodi ili watanzania waweze kuujua zaidi.

Wakizungumza leo, Oktoba 21,2021 katika  kikao cha kuwajengea uwezo Makatibu Tawala wa Mikoa 26 namna bora mfumo wa Postikadi,wamesema elimu inahitajika zaidi kwa wananchi ili waweze kuujua vizuri mfumo huo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Ngusa Samike amesema mfumo wa anwani za makazi katika Jiji la Mwanza umefanikiwa kwa sababu walitoa elimu juu ya mfumo huo.

Amesema wameweza kuweka mfumo huo katika Kata 16,Mitaa 174 ambapo jumla ya watu 485,000 wamefanikiwa kuwafikia ambapo amedai mafanikio waliyopata ni pamoja na kuweza kupata huduma mbalimbali mahali unapoishi  ikiwemo kuletewa chakula nyumbani.

Katibu Tawala huyo wa Mwanza amesema wamekabiliwa na changamoto za  matumizi yasiyosahihi,uharibifu wa mindombinu, ajali nguzo kugonjwa pamoja na zoezi la kupendekeza majina kila mmoja kuwa kutaka jina lake ndio liwekwe.

Kwa upande wake,Katibu Tawala wa  Mkoa wa Dodoma,Dk.Fatma Mganga amesema mfumo ni mzuri lakini zinahitajika nguvu za ziada kwani kasi ni ndogo ambapo amedai mfumo huo unaongeza ustaarabu.

Naye, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera,Profesa Faustian Kamuzora amesema bado inahitajika elimu kuhusu postikodi kwani wengi hawana uelewa ambapo amedai wakielimishwa hasa makatibu tawala watakuwa na uelewa mkubwa kuhusiana na jambo hilo.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Angelina Lutambi,amesema kuna haja ya fedha zinazotakiwa kutolewa na baadhi ya Halmashauri kwa ajili ya kuweka mifumo ya Postikodi zikagawanywa na kutolewa kwa Halmashauri zote.

Kikao hicho kiliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Dk. Zainabu Chaula kwa kushirikiana na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Profesa Riziki Mdoe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles