27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Makamba atakiwa kutimiza ahadi ya kuwasha umeme vijiji vyote Morogoro

Na Ashura Kazinja, Kilosa

Waziri wa Nishati, Januari Makamba ametekiwa kutimiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa umeme wa REA unawaka katika vijiji vyote vya mkoa wa Morogoro ifikapo Aprili, Mwaka huu.

Katibu Mkuu CCM Taifa, Daniel Chongolo akizungumza na wakazi wa kata ya Dumila Wilayani Kilosa (hawapo pichani) akiwa kwenye ziara ya siku tisa mkoani hapa.

Agizo hilo limetolewa leo Januari 30, 2023 na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chongolo katika Kijiji cha Dumila Juu kata ya Dumila baada ya kupokea kero ya umeme kwenye maeneo mbalimbali mkoani hapa ikiwemo Dumila Juu, wakati akiwa kwenye ziara yake ya siku tisa mkoani hapa ya kukagua miradi na shughuli za maendeleo pamoja na kuangalia uhai wa Chama.

“Nimugize Waziri wa Nishati, Januari Makamba kutekeleza ahahdi yake aliyoitoa ya kuhakikisha kwamba umeme unawaka ifikapo Aprili, mwaka huu. Pia nilipokea malalamiko kutoka kwa wananachi juu ya ukosefu wa umeme katika vijiji 60 vilivyopo chini ya mradi wa maji kupitia mradi wa usambazaji nishati vijijini (REA) awamu III mzunguko 2.

“Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alitenga na kuleta fedha mkoani Morogoro kwa ajili ya kupatikana umeme katika vijiji mbalimbali ili kuleta maendeleo kwa wananchi na alipomuuliza Waziri Makamba aliahidi kuwasha umeme katika vijiji vya Morogoro ifikapo mwezi Aprili mwaka huu, hivyo ahahidi hiyo aitimize,” amesema Chongolo.

Akizungumzia kuhusu umeme Meneja wa TANESCO Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Fadhili Chilombe amekiri vijiji 55 kati ya 60 kutokuwa na umeme kwa wakati uliopangwa kufuatia Mkandarasi mwenye kampuni ya HNXJDL INT CONTRUCTORS kutokuwa na utekekezaji mzuri wa mradi huo.

Meneja wa REA Taifa Mhandisi Romanus Lwena akizungumzia kuhusu juhudi wanazofanya kuhakikisha umeme unaingia kijijini hapo.

“Sisi TANESCO tutahakikisha kazi hiyo inakamilika na vijiji vyote vinavyohusika kupata umeme kwa wakati licha ya mkandarasi kushindwa kukamilisha usambazaji tangu Agosti mwaka 2021 aliposaini mkataba hadi kuonekana kushindwa kukamilisha itakapofika mwisho wa mkataba wake Februari 28, mwaka huu,” a,mesema Mhandisi Chilombe.

Mhandisi Chilombe amewahakikishia wananchi wa vijiji 60 vya kata ya Dumila kuwapunguzia bei ya gharama za huduma za umeme kutoka 321,000 ya sasa hadi kufikia 27,000 inayopaswa kulipia kupitia REA.

Mhandisi Chilombe amewaasa wananchi wa vijiji hivyo kuwa tayari kibadilishiwa gharama ya huduma hiyo pale kata hiyo itakapopewa hadhi ya kuwa mji mdogo sababu kuwa mji mdogo ni sehemu ya kuonekana kukua katika kila nyanja ikiwemo kiuchumi.

“Wapo watu wanakaa kwenye miji lakini hawana hadhi hiyo na wanaendelea kulipa gharama kubwa za kuingiza umeme, mkishapata hadhi ya kuwa mji mdogo nitarudi tena kuangalia vijiji vyenye hadhi na kuwarudisha kwenye huduma kubwa ya kuingiziwa umeme,” amesema Mhandisi Chilombe.

Awali, Mwenyekiti wa shina namba 10 Balozi Bakari Kimario alimuomba Katibu Mkuu huyo kuipa hadhi ya mji mdogo kata ya Dumila kutokana na kuendelea kukua kwa kasi kila kukicha.

Pia amemuomba awasaidie ili wapunguziwe gharama kubwa za kuingiza umeme kwa sababu ni changamoto kubwa kwao katika kupiga hatua za maendeleo.

Katika mkutano huo wa hadhara Mwenyekiti wa Jimbo la Mikumi Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bakari Hassan amerejea CCM akidai kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Dk. Samia ambaye anaonesha njia ya maendeleo kiuchumi na kisiasa kwa vyama vyote ambapo haoni sababu ya kuendelea kuwa CHADEMA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles