31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Chongolo atoa siku saba kwa Waziri Bashe kufika Kilosa

Na Ashura Kazinja, Kilosa

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chongolo amempa siku saba Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kufika katika Kijiji cha Mvumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro kuhakikisha skimu ya umwagiliaji iliyopo Mvumi na zingine za mkoa mzima zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Katibu Mkuu CCM Taifa, Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mvumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Chongolo ametoa agizo hilo leo Januari 30, 2023 katika kijiji cha Mvumi kata ya Mvumi wilayani Kilosa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku tisa mkoani humo.

Amesema katika kijiji hicho kuna skimu ya umwagiliaji ambayo haifanyi kazi huku kukiwa na uongozi usio sahihi.

Hivyo, amemuagiza Waziri Bashe kuhakikisha anaweka Mameneja kwenye kila skimu za umwagiliaji mkoa ili waweze kutoa huduma za karibu na kuepusha migogoro ikiwemo ya mipaka kwa wakulima na wafugaji.

“Ninamuagiza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe afike hapa na ahakikishe anaweka mameneja kwenye kila skimu za umwagiliaji, hii itasaidia watoe huduma kwa karibu ikiwamo pia kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji,” amesema Chongolo.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Mercy Maneno amesema licha ya kuwa na ardhi nzuri na ya rutuba lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mazao kulingana na kilimo kutokana na kukosa mabwawa makubwa ya kuhifadhi maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Katibu wa siasa na uenezi NEC Sophia Mjema akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mvumi.

Naye Katibu wa Siasa, Iitikadi na Uenezi(NEC), Sophia Mjema amewataka wananchi, wanachama na wapenzi wa CCM kuendelea kutangaza sera na Ilani ya chama hicho kwa kutangaza mazuri yote aliyofanya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kwa sasa Tanzania kuna shule nzuri ambazo wanafunzi wengi hupata elimu bure kuanzia darasa la sifuri hadi kidato cha sita mambo ambayo amesema kuwa yote ni mipango na utekekezaji Ilani ya Chama.

Pia ameishauri jamii na wanachama na wasio wanachama wa chama hicho kukaa tayari kusubiri mafunzo ya sera na itikadi ya CCM yatakayotolewa hivi karibuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles