25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAKALLA-MKIACHA RUSHWA UCHUMI UTAKUWA  

Na PENDO FUNDISHA-MBEYA


makalaSERIKALI mkoani Mbeya, imesema uchumi wananchi unaweza kukua kwa haraka, endapo baadhi ya watumishi wa umma ambao si waadilifu wataepuka vitendo vya urasimu.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla wakati wa maadhimisho ya siku ya maadili, haki za binadamu, uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa.

Alisema jitihada za Serikali katika kuhakikisha uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla unakua haraka,  huenda zisifanikiwe kutokana na kukithiri kwa vitendo vya urasimu, vinavyodaiwa kufanywa na viongozi ama maofisa wa Serikali.

“Wananchi wanakutana na changamoto nyingi mno, wakati wa mchakato wa huanzishwaji wa biashara au wanapohitaji huduma fulani,  mtumishi anajifanya ana mambo mengi ya kufanya, yote kwa yote anatengeneza mazingira ya mwananchi kuona ugumu wa suala lake na kuanza kushawishi  kutoa rushwa na mtendaji kuipokea, kwa kweli hili hatutalivumilia,”alisema.

Kutokana na hilo, Makalla aliwataka wananchi kuisaidia Serikali kujenga misingi bora ya maadili kwenye jamii na watumishi wa umma kwa kuwafichua watendaji wasio waadilifu na wala rushwa.

Alisema endapo watatoa ushirikiano wa kutosha kwa taasisi mbalimbali za Serikali kwa kufichua vitendo vya ukiukwaji wa maadili unaofanywa na watumishi wa umma,jitihada za kukuza uchumi zitafanikiwa.

“Kama haya hayatafanyika wananchi watakosa imani kwa watumishi wa umma na hatimaye Serikali yao na shughuli za umma kuendeshwa bila ya kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na taratibu,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles