28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Makala| Nafasi ya Uzazi wa Mpango katika kuimarisha lishe ya jamii

Na Yohana Shida, Geita

Kwa mjibu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), nchini Tanzania shughuli za lishe zilianzishwa na Wizara ya Afya mnamo miaka ya 1950 kutokana na ripoti zilizoonyesha ongezeko la ukubwa wa vifo.

Pia sababu nyingine ni ongezeko la magonjwa mbalimbali, tukio la njaa na uwepo wa vichocheo vingine ambavyo vilichangia ukuaji wa udumavu.

Ofisa Lishe Mkoa wa Geita, Riziki Mbilinyi 

Jitihada kubwa zilichukuliwa katika kupambana na kila hali kama vile kuzorota kwa hali kubwa ya afya katika idadi ya kundi la aina fulani la watu. 

Zaidi ya hayo mfumo wa ushirikiano wa sekta-mtambuka ilitumika na kupelekea maendeleo ya kuundwa kwa Kamati ya Ushauri ya Sekta-Mtambuka lengo lake kuu lilikuwa ni kutoa ushauri katika masuala mbalimbali ya lishe.

Hali ya lishe mkoani Geita

Akizungumuza katika mawasilisho ya mkataba wa lishe mbele ya Mkuu mkoa wa Geita, Ofisa Lishe wa mkoa, Riziki Mbilinyi anasema kwa sasa tatizo la udumavu wa watoto mkoani Geita ni asilimia 38.9.

Anasema kiwango hicho ni sawa na takribani watoto laki moja ambapo tathimni ya sita ya kitaifa ya mkataba wa lishe ya mwezi Septemba 30, 2022, inaonyesha Geita imeshika nafasi ya pili kutoka mwisho 

“Ukiangalia kwa mwaka jana 2021/2022 takribani halmashauri nne za mkoa wa Geita hazikupanga bajeti kwa ajili ya watoto chini ya miaka mitano, ambayo ni Sh 1,000 kwa kila mtoto.

“Lakini vilevile hata kwenye matumizi halmashauri nne hizo hizo zimejikuta kwamba hazijatumia Sh 1,000 kwa kila mtoto,” anasema na kuongeza.

“Ukiangalia kwenye matumizi ya fedha halmashauri ambayo angalau ilifanya vizuri ni halmashauri ya mji wa Geita na halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale.

“Halmashauri nne zilizobaki hazikufanya vizuri, yaani hazikutumia Sh 1,000 kwa mtoto, zilitumia chini ya Sh 1,000 na halmashauri hizo ni Bukombe, Chato, Mbogwe na Halmashauri ya wilaya ya Geita,” anasema.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo.

Anasema ofisi ya mkuu wa mkoa idara ya lishe inaendelea kuangalia viashiria vya tatizo la lishe na kupima kila robo ya mwaka katika ngazi ya halmashauri na mkoa kupitia vikao vya tathimini.

“Kigezo kilichotufanya tukashindwa kufikia malengo ni kigezo cha fedha, kwa sababu ukiangalia vigezo vyote tumefanikiwa kwa asilimia 80 lakini kwenye kigezo cha fedha tumefanikiwa kwa asilimia 50 tu,” anasema.

Mikakati ya Kuimarisha Lishe mkoani Geita

Ili kuimarisha lishe ndani ya mkoa Riziki anasema “Tutahakikisha tunapeleka elimu kwa wananchi, kupitia kamati za chini kwa maana ya kamati ya maendeleo ya kata na kamati za huduma za jamii,” anasema.

Anasema kupitia kamati ya huduma ya jamii watahakikisha fedha ikiyotengwa kwa idadi ya watoto inawafikia walengwa ka maana ya kuhudumia kundi la watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Riziki anaeleza, pia wamejipanga kusimamia suala la mlo kamili ngazi ya kaya, liweze kuzingatiwa ili kuondokana na tatizo la udumavu na kusababisha kushuka kwa afya na utapiamulo wa watoto.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita wa Geita, Martin Shigela alielekeza wakurugenzi wa halmashauri kuchukua hatua stahiki kumaliza tatizo la udumavu wa watoto kwenye maeneo yao.

Shigela anasisitiza suala la bajeti ya halmashauri kwa ajili ya lishe ni suala la lazima na siyo ombi na kwa kufanya hivo utekelezaji wa sera na mipango ya kuimarisha lishe ndani ya mkoa itaweza kufanikiwa.

Aidha Shigela anawataka maofisa lishe kutimiza wajibu wao kuwafikia wananchi kuwapatia lishe na kuondoa dhana potofu na malezi duni yanayochangia watoto kukua katika mazingira hatarishi.

Nafasi ya Uzazi wa Mpango katika kuimarisha lishe

Akizungumuza baada ya kikao cha mapitio ya mkataba wa lishe halmashauri ya mji, Mkuu wa Wilaya Geita, Wilson Shimo anawashauri wananchi wilayani humo kuzaa idadi ya watoto wanaomudu.

Shimo anasema suala la lishe litafanikiwa ngazi ya familia iwapo wazazi watakuwa na idadi ya watoto wanaoweza kuwahudumia mahitaji muhimu ambayo ni malazi, mavazi na chakula.

Anasema serikali inafanya kazi kubwa kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu na kwamba maendeleo ya elimu yatafikiwa iwapo wazazi nao watatimiza wajibu wao kwa watoto. 

“Rai yangu kwa watanzania na wana Geita wenzangu, tuendelee kuwa na mpango ambao utasaidia kuwa na watoto tunaoweza kuwasomesha, tunaweza kuwatunza, tunaweza kugharamia matibabu yao,” anasema Shimo.

Aliongeza pia kuwa na idadi ya watoto unaowamudu itawezesha kuimarisha ulinzi na maadili kwa watoto na kupunguza ama kuondoa tatizo la watoto kuishi katika malezi hatarishi kwa tabia na afya zao.

Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe Halmashauri ya Mji wa Geita, Dk. Konkamukula Clemence

Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe halmashauri ya mji wa Geita, Dk. Konkamukula Clemence anasema mafanikio ya suala la lishe ataenda sambamba na uzazi wa mpango.

Anasema ajenda ya masuala ya lishe ni lazima iambatanishwe na uzazi wa mpango kufanikisha mabadiliko ya lishe ndani ya jamii na kuondokana na tatizo la udumavu wa watoto.

“Uzazi wa mpango si idadi ya watoto pekee bali ni namna ya kupitanisha watoto kutoka mmoja hadi mwingine, huyu akue alelewe vizuri, afikie pahala fulani, ndio apatikane mwingine kwa wakati muafaka,” anasema Dk. Clemence. 

Anasema hayo yote ni kutokana na ukweli kwamba idadi ndogo ya watoto ndani ya familia inamupa nafasi mzazi ama mlezi kuweza kuwalea watoto na kuwapatia mulo kamili kadri ya mahitaji.

Dk. Clemence anasema uwepo wa vituo vingi vya kutolea huduma ndani ya halmashauri imewezesha ajenda ya uzazi wa mpango kuanza kueleweka ndani ya jamii na sasa mwitikio unazidi kukua.

Anakiri iwapo jamii itaendelea kuongeza mwitikio wa kuzaa kwa mpango ni wazi kwamba hata suala la lishe kuanzia ngazi ya kaya, halamshauri na hata mkoa litaweza kuimarika kadri ya malengo.

Naye Ofisa Lishe Halmashauri ya Mji wa Geita, Timotheo Mwendi anasema tathimini inaonyesha tatizo la udumavu wa watoto ndani ya halmashauri limepunguampaka kufikia asilimia 0.1 pekee.

Anakiri matumizi ya uzazi wa mpango yana nafasi kubwa kuimarisha lishe na utimamu wa afya ya mama na mtoto kwani bado kina mama wanakutana na changamoto za kiafya kutokana na kuzaaa mfululizo.

Anasema mama akiweza kuzaa kwa mpango inamusaidia kupata nafasi ya kuimarisha afya yake a kumtunza mtoto aliyenaye kabla ya kujifungua mtoto mwingine.

Mtazamo wa Wazazi

Jenifer Haule (34) mama wa watoto wanne, mkazi wa mtaa wa Miti mirefu mjini Geita anasema kila mzazi anatamani kumuona mtoto akipata lishe bora lakini changamoto kubwa ni gharama ya chakula.

Anaeleza kuwa uwepo wa watoto wengi ndani ya familia ndio kikwazo kikubwa cha kupata mulo kamili na lishe bora kwani kadri watoyto wanavyoongezeka ndio gharama za kuwahudumia zinaongezeka.

Jenifer anakiri kwamba, huduma ya chakula chenye lishe ndani ya familia yake ilikuwa ni ya uhakika kipindi akiwa na watoto wawili ikilinganishwa na sasa ambapo anamefikiisha watoto wanne.

Naye Juma Majogoro,  baba wa watoto watatu anasema ukiwa na watoto wachache kwa maana ya wawili ama watatu kama baba utamudu angalau kuwachukulia watoto matunda kila siku utokapo kazini.

Anasema wakati mwingine kina baba wanazidiwa na mahitaji ya watoto na wao kushidnwa kutoa huduma bora ya chakula kwa watoto na hivo kuishia kuwekeza kwenye uwingi wa chakula na siyo ubora.

Juma anasema ni kweli kama vijana wanaoanza maisha watahamasika kutumia uzazi wa mpango wana nafasi kubwa ya kuwalea watoto wanaowazaa kwa kuwatimia mahitaji kamili ya chakula na malazi. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles