NA BADI MCHOMOLO, DAR ES SALAAM
MSANII wa muziki wa hip hop nchini, Songalael Mwangala ‘Songa’, amedai kwamba kuachia albamu kunampa faida kubwa.
Msanii huyo kutoka kundi la Tamaduni Music, amesema ataendelea kuachia albamu kwa kuwa zinampa faida kubwa tofauti na kuachia nyimbo moja moja.
“Kuna wasanii ambao wanaamini kuwa albamu hailipi, lakini kwa upande wangu ninaamini inanilipa kwa kiasi kikubwa, kwanza inanipa jina ndani na nje ya nchi,” alisema Songa.
Hata hivyo, msanii huyo amejipanga kuachia wimbo kila wiki ndani ya mwezi mmoja na nusu kwa kuwa ana nyimbo nyingi katika maktaba yake.
Msanii huyo kwa sasa anatamba na albamu yake mpya ambayo inajulikana kwa jina la ‘Hisia za Moyoni’.