30.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: marufuku saruji ya nje kuingia nchini

Amina Omari – Tanga

Serikali imesema haitaruhusu saruji inayotoka nje ya nchi kuingia nchini ili kuwalinda wazalishaji wa ndani.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumanne Machi 3, alipotembelea katika kiwanda cha kuzalisha saruji cha Tanga.

Amesema kwa sasa nchi inajitosheleza kwa saruji inayozalishwa nchini na ziada inafanya vizuri katika masoko ya nje.

“Tutakachofanya ni kuleta mabehewa kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji wa shehena za saruji kwa njia ya treni kwa ajili ya unafuu wa soko,” amesema Majaliwa.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Reinhardt Swart amesema kuwa miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni umeme na gharama za usafirishaji.

“Usafirishaji wa kutumia magari una gharama kubwa licha ya kuingia makubaliano na shirika la reli nchini lakini bado kumekuwa na uhaba wa mabehewa ya kusafirisha shehena ya  saruji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles