Madee kumpa uhuru mwanawe

0
717

Glory Mlay

MWANAMUZIKI wa bongo fleva, Hamad Ally ‘Madee’ amesema iwapo mwanawe wa kike, Aimal Hamad, atachagua kuwa msanii litakuwa ni jambo la kawaida.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Madee alisema kuwa atamruhusu kufanya muziki kwasababu hata yeye amefuata nyayo za baba yake katika fani hiyo.

Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi kwenye Sanaa kwa wanawake lakini hana budi kumruhusu kuonyesha kipaji chake kwa kuwa kila mtu amepangiwa ridhiki yake.

“Wazazi wanashauriwa kuwaangalia watoto wao wafanye kitu wanachotaka, hivyo siwezi kumpangia mtoto wangu  kitu cha kufanya katika maisha yake, akitaka muziki sawa, akitaka kuwa yeyote ni yeye na maisha yake,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here