Elimu ya matumizi dawa za usingizi yatolewa

0
665

MWANDISHI WETU – MBEYA

Wataalamu wa dawa za usingizi katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mbeya wamepewa mafunzo ya matumizi ya dawa hizo ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza wakati wa utoaji huduma hiyo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku tatu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Salum Manyata amesema wataalamu hao wanajukumu kubwa la kuboresha utoaji wa huduma za dawa za usingizi kwa kina mama wajawazito wakati wa upasuaji.

“Ni vema washiriki wakatumia fursa hii walioipata ya mafunzo ya  kujengewa uwezo ili kutekeleza yale ambayo wameyapata kwa kutoa huduma salama na sahihi kwa wajawazito.

Dk. Manyata amewaasa wataalamu hao kupeleka mrejesho wa masuala mbalimbali mapya waliyoyapata kwa wengine katika vituo vyao watakaporejea ili kuhakikisha taratibu zote zinasimamiwa vizuri.

Mafunzo hayo yanatolewa na wakufunzi kutoka ndani na nje ya nchi na kushirikisha wataalam 35 wa dawa za usingizi kutoka Nyanda za Juu Kusini na kufadhiliwa na Chama cha Madaktari Bingwa  wa dawa za usingizi duniani (WFSA) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa  wa dawa za usingiizi Tanzania (SAFE) kwa malengo ya kuwajengea uwezo watoa huduma ya dawa ya usingizi katika vituo vya afya na hospitali .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here