21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA ATAKA MADINI YALETE TIJA

Na EVANS MAGEGE

WAZIRI  Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema kuna ulazima mkubwa kwa nchi za Afrika kuandaa rasilimali watu, maarifa na vitendea kazi ili kuifanya sekta ya madini iwe na tija ndani ya mataifa husika.

Majaliwa alisema hayo Dar es Salaam jana, wakati wa  mkutano wa 37 wa Baraza la Uongozi wa Kituo cha Madini, Kijiosayansi cha Afrika(AMGC).

Alisema viongozi wanapaswa kuweka mazingira rafiki ya kuvutia uwekezaji na uendelezaji kwenye eneo la madini kwa lengo la kuhakikisha rasilimali hiyo inasukuma uchumi wa nchi.

“ Changamoto kuu kwa sasa ni jinsi gani tunaweza kuwa na sekta ya madini inayotoa mchango stahiki katika nchi husika na Bara la Afrika kwa ujumla.

“Tunaweza kusimamia sekta hii kwa kuwafanya wananchi wetu hususani katika maeneo yenye hizi rasilimali wakanufaika na kuona fahari kuwa nazo, ni lazima sehemu zenye madini zifanane na madini badala ya kuacha mashimo, umasikini na mateso kwa wananchi,” alisema Majaliwa.

Alisea zaidi ya miongo minne iliyopita, waasisi wa mataifa ya Afrika walifikiri wazo la kuwa na kituo cha kujenga uwezo  wa wataalamu wa kusimamia sekta ya madini hivyo wakaamua kujenga kituo cha AMGC.

Alisema kituo hicho, kimetimiza miaka 40 na uanzishwaji wake ulifadhiliwa na Kamisheni ya Uchumi ya Afrika chini ya Umoja wa Mataifa(UNECA).

“ Lengo la uanzishwaji wa kituo hiki ni kuhakikisha sekta ya madini inawajibika kuleta maendeleo ya kijamii na uchumi pia ikijali masuala ya mazingira.

“ Kituo hiki kinafanya tafiti, kinafundisha wataalamu na pia kina maabara ya kisasa kwa ajili ya uhakiki na uongezaji thamani ya madini,” alisema Majaliwa.

Alisema  kituo hicho kikitumika vyema kwa mujibu wa kusudio la uanzishwaji wake kinaweza kutoa tija kubwa kwenye sekta ya uchimbaji wa madini, uongezaji wa thamani na usimamizi wa sekta ikiwamo usimamizi wa mazingira.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati na Madini ambaye pia ni Mwenyekiti wa AMGC, Dk. Medadi Kalemani alisema kituo hicho kilianzishwa na kazi yake ilikuwai kutoa elimu, kutathimini na kutoa madini kiwango kidogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles