30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa apokea msaada wa Sh bilioni 1.18 kukabili corona

Mwandishi wetu -Dar es Salaam

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amepokea msaada wa fedha na vitu mbali mbali kwa ajili ya kukabiliana na homa kali ya mapafu inaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) wenye thamani ya sh. bilioni 1.185.

Akipokea msaada huo jana katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyoko Magogoni, jijini Dar Es Salaam, Majaliwa aliwashukuru wadau hao na kuwataka Watanzania waendelee kushirikiana na Serikali katika hatua zinazochukuliwa kukabiliana na ugonjwa huo.

Amewataka Watanzania wote waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ili kuzuia usisambae zaidi nchini.

“Hii ni vita kubwa inahitaji tupigane kwa lengo la kuzuia janga hili lisisambae zaidi nchini, hivyo tuzingatie maagizo ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ya kumtaka kila Mtanzania ashiriki kwenye vita hii,”alisema Majaliwa.

Miongoni mwa wadau waliotoa msaada huo ni benki ya UBA Tanzania  iliyotoa Sh milioni 230, CRDB Sh milioni 150 na  NMB Sh milioni 100.

Wadau wengine ni  Karimjee Jivanjee Ltd na kampuni zake tanzu Sh milioni 200 na kuhaidi kufanyia matengenezo magari yote ya toyota yanayotumika katika kukabiliana na COVID-19 kwa muda ya siku saba bure, na  jenereta la KVA 180 lenye thamani ya sh. milioni 75.

Baada ya kupokea misaada hiyo, Majaliwa aliwashukuru wadau hao kwa vitu walivyovitoa kwa ajili ya kupambana na COVID-19.

Alisema Serikali kwa upande wake inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kupambana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hausambai zaidi nchini.

Kuhusu wadau wengine wanaohitaji kutoa misaada, alisema ofisi yake iko wazi pia wanaweza kupeleka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwa wanalio nje ya nchi au sehemu yoyote wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti  yenye Jina la: National Relief Fund Electronic  Akaunti Na: 9921159801

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles