28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Operesheni maalumu ya wezi wa magari yanasa 128

Ramadhan Hassan -Dodoma

KUTOKANA na ongezeko la wizi wa magari na pikipiki  nchini, Jeshi la Polisi limeanzisha oparationi ya kuwasaka wezi hao ambapo hadi sasa linawashilikia watu 128 kwa wizi wa magari 130.

Pia limewataka wanaonunua magari yaliyototumika nchini, wajiridhishe kama muuzaji ndiye mmiliki halali  kwa kutumia polisi kukagua gari hilo na kuonanisha za kadi yake na kumbukumbu za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

Hayo yalielezwa jana Jijini hapa na Mkurugenzi wa Upelelezi Nchini (DCI) Robert Boazi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

Alisema  kwa sasa kumekuwa na ongezeko la wizi wa magari,  pikipiki na vipuri vyake.

Alisema kutokana na hali hiyo, jeshi hilo limeanzisha operation maalum ya kukabiliana na wizi huo ambapo hadi sasa wamekamata magari 130, pikipiki 193, vipuri 753 na watuhumiwa 128.

“Tumeshuhudia wizi wa magari ama kuibiwa vifaa vyake taa na vitu vingine na mara nyingi matukio hayo yanafanyika  usiku.

 “Nitoe wito kwa wananchi wanaonunua magari ambayo yametumika, jambo la kwanza ni kukagua gari polisi ili kuoanisha nyaraka za injini kama zinaendana na kadi ya gari, pia kuangalia kama nyaraka zilizoleta gari kutoka nje ya nchi ni halali. Kwa kufanya hivyo itapunguza wimbi la wizi wa magari.

Alisema mtu akitaka kufanya  mabadiliko katika gari anapaswa kutoa taarifa TRA ili kumbukumbu ziweze kuingizwa.

 “Mtu anapotaka kufanya mabadiliko katika gari anapaswa kutoa taarifa TRA ili kumbukumbu ziweze kuingizwa kwa sababu tunaona watu wananunua spea, injini na bodi na anabadilisha rangi bila kufuata taratibu na mwisho wa siku tukifanya operation lazima tuwakamate,’’alisema.

WAUZAJI WA VIPURI VYA MAGARI

Boazi alisema wauzaji wa vipuri vya magari na pikipiki vilivyotumika ni lazima wazingatie sheria na kwamba polisi wana mamlaka ya kukagua gereji na maduka ya vifaa chakavu ili kujiridhisha kama ni halali.

Pia, alitoa wito kwa wananchi wanapoibiwa simu kutoa taarifa mapema kwani jeshi hilo kwa sasa lina vifaa vya kisasa vya kutambua simu ilipo.

“Simu inapoibiwa ni waombe wananchi waripoti polisi, tuna timu nzuri sana ya kuweza kufuatilia kama simu imeibiwa na kujua kama ni yako ama sio yako, ukiibiwa ripoti polisi,”alisema.

Katika hatua nyingine Boazi alisema hali ya usalama ni nzuri kwa Januari hadi Februari mwaka huu, ambapo makosa yamepungua kwani katika kipindi hico mwaka jana yalikuwa 9,572  na mwaka huu nni 9,263.

Kwa upande wa usalama barabarani, alisema mwaka jana kulikuwa na makosa  533 ambapo Januari hadi Februari  mwaka huu yamefika  425.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles