27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa amwakilisha Rais Magufuli London  

KassimNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameondoka nchini jana kwenda London, Uingereza kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi unaojadili suala la kupambana na rushwa (Anti-Corruption Summit 2016).

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam  jana, Majaliwa alisema anamwakilisha Rais Dk. John Magufuli kwa sababu, atahudhuria sherehe za kuapishwa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

“Rais Dk. Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), siku hiyo hiyo, mmoja wa marais wa nchi wanachama anaapishwa. Kwahiyo amelazimika kwenda kuhudhuria sherehe hizo,” alisema Majaliwa.

Kuhusu mada ya mkutano huo, Majaliwa alisema Tanzania inafanya vema katika mapambano dhidi ya rushwa na kwamba baadhi ya nchi zimeanza kuvutiwa na juhudi ambazo Serikali imekuwa ikichukua.

“Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ameandaa mkutano huu na alimwalika Rais Magufuli ili ahudhurie, akiwa ni miongoni mwa wakuu wa nchi 60 watakaohudhuria mkutano huo. Tanzania ni miongoni mwa nchi mbili kutoka bara la Afrika ambazo zimealikwa kushiriki. Nchi nyingine ni Nigeria,” alisema.

Majaliwa atafuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola, wataalamu wa sekta ya rushwa na wanasheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles