27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AKARIBISHA WACUBA KUJENGA VIWANDA

Na MWANDISHI  MAALUM

-HAVANA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba hapa nchini, Lucas Polledo, ambapo amewakaribisha wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja kuwekeza nchini katika viwanda vya dawa.

Alisema kwa sasa Serikali ya Tanzania inaagiza dawa kutoka nje ya nchi jambo ambalo linasababisha kutumia fedha nyingi, hivyo uwepo wa kiwanda utasaidia kupunguza gharama. Pia wawekezaji watakuwa na uhakika wa soko la bidhaa zao.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Balozi Polledo mjini Havana. Majaliwa yuko Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Alisema Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda nchini kama mkakati wa kukuza uchumi na kufikia uchumi wa kati, hivyo wafanyabiashara kutoka nchini Cuba wanakaribishwa kuja kuwekeza nchini, hususani katika viwanda vya dawa na sukari.

Waziri Mkuu alisema licha ya Tanzania kuwa ni nchi ya amani na yenye utulivu wa kisiasa, pia imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji, jambo ambalo litawawezesha watakaokuja kuwekeza nchini.

Pia alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Cuba kwa ushirikiano mzuri na Serikali ya Tanzania kwa sababu Cuba ni mojawapo kati ya nchi zenye ushirikano wa muda mrefu na Tanzania.

“Tanzania na Cuba zina historia ya kutosha. Tunatambua mahusiano mazuri yaliyopo kati nchi zote mbili, ambayo yalikuwepo kuanzia Serikali ya awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere,” alisema Majaliwa.

Kwa upande wake, Balozi Polledo alisema Serikali ya Cuba itahakikisha uhusiano wake na Serikali ya Tanzania unaendelea kuimarishwa.

Pia alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo pamoja na kukuza uchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles