30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

LOWASSA AMTEMBELEA BULAYA MUHIMBILI

 

MARGRETH MWANGAMBAKU(TUDARCO)

Na TUNU NASSOR

-DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Edward Lowassa jana alikwenda kumjulia hali Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya ambaye amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Bulaya amelazwa wodi namba 18 Sewa Haji baada ya kufikishwa hospitalini hapo Agosti 21, mwaka huu saa tano usiku akitokea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.

Hali ya mbunge huyo ilibadilika ghafla alipokuwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime baada ya kuugua akiwa mahabusu kwenye kituo cha polisi Tarime alipokuwa ameshikiliwa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa Chadema Tumaini Makene alisema Lowassa alikwenda Muhimbili kumjulia hali Bulaya jana mchana.

“Taarifa nilizonazo ni kwamba mzee (Lowassa) amekwenda kumwona na kumjulia hali Bulaya Muhimbili mchana wa leo (jana),” alisema Makene.

Naye Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, John Stephen alisema Lowassa amemtembelea Bulaya wodini hapo asubuhi ya jana na kwamba afya yake imeendelea kuimarika.

“Hata mimi nimetoka kumwona Bulaya muda si mrefu nimemkuta yupo vizuri, ameweza kula mwenyewe na kutembea bila kusaidiwa,” alisema John.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles