32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mahiza awaasa Watanzania umuhimu wa kupiga kura

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

MWANGALIZI wa ndani wa uchaguzi wa Tanzania mwaka huu,Mwantumu Mahiza ameshauri uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Watanzania wasiishie kujiandikisha kama mwaka huu, bali wanatakiwa kwenda kupiga kura.

Hatua hiyo, imekuja kutokana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusema zaidi ya watu milioni 29 walijiandikisha katika daftari la kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu, lakini waliopiga kura milioni 15 pekee ndiyo waliopiga kura.

Akizungumza jijini Dodoma jana

baada ya utoaji wa cheti cha ushindi kwa mgombea wa CCM, Rais Dk.John Magufuli Mahiza alishauri uchaguzi ujao Watanzania wasiishie kujiandikisha kama mwaka huu, wanatakiwa kwenda kupiga kura kwa sababu watakuwa natumia haki yao ya msingi na kupunguza gharama ya vifaa vingi vinavyoandaliwa bila kutumia.

“Tunaushauri uchaguzi unaokuja wananchi wasiishie kujiandikisha tu bali waende wakapige kura kwani kupiga kura ni kutoa sauti yao wasipopiga kura wanaacha sauti za wengine,”alisema Mahiza.

Alisema wanshukuru kwa uchaguzi wa mwaka huu kufanyika kwa amani na

kwa ulifuata kanuni na sheria.
“Kwa niaba ya timu ya waangalizi

wa ndani, tunachukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwa namna mchakato ulivyoonda,tunaipongeza tume, umeonekana uchaguzi kwa nchi nzima ulikuwa na mambo mazuri,kanuni na sheria zilifuatwa na taratibu zilizingatiwa.

“Kwa niaba ya timu ya watazamaji, tunaomba kusisitiza ulivyoanza kwa kumtegemea Mungu tuendelee kumtegemea kwa sababu mmalaka yanatoka kwake.Uchaguzi umefanyika aliyepaswa kupata amepata na leo (jana), ametunukiwa tunaomba turidhie na tuendelee,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles