Na RAMADHAN HASSAN -DODOMA
MFUMUKO wa bei kwa mwezi ul- ioishia Aprili umepungua hadi asil- imia 3.3 kutoka asilimia 3.4 Machi huku mahitaji ya baadhi ya bidhaa kama malimao na vitunguu swau- mu yakiongezeka.
Hatua ya kuongezeka kwa ma- hitaji ya bidhaa hizo inaweza ikawa imesababishwa na virusi vya co- rona ambapo baadhi ya Watanzania wamekuwa wakitumia vitu hivyo kama sehemu ya tiba na kinga.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana jijini Dodoma jana, Mkurugezi wa Sensa za Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Min- ja, alisema mwaka ulioishia mwezi Aprili mahitaji ya bidhaa hizo ya- meongezeka.
“Matumizi yake yamekuwa
yapo juu lakini ni kwa mwezi ulioi- sha April na sio kwa mwaka,”alisema Minja. Alisema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Aprili umepungua hadi asilimia 3.3 kutoka asilimia 3.4 kwa Machi mwaka huu.
Alisema hii inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili imepungia ikilingan- ishwa na bei za mwezi Aprili.
Alisema kuongezeka kwa mfu- muko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bid- haa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha kilichoishia Aprili 2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Aprili mwaka 2019.
Alisema bidhaa za vyakula zi- lizopungua bei ni pamoja na unga wa ngano kwa asilimia 1.4 matunda kwa asilimia 6.8, viazi vitamu kwa asilimia 5.5 na ndizi za kupika kwa
asilimia 7.9.
“Kwa upande mwingine baa-
dhi ya bidhaa zisizo za vyakula zi- lizopungua bei ni pamoja na mafuta ya taa kwa asilimia 4.6, dizeli kwa asilimia 7.2 na petroli kwa asilimia 3.8,”alisema.
Vilevile alisema mfumuko wa bei kwa bidhaa za vyakula na viny- waji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili 2020 umepungua hadi asilimia 4.6 kutoka asilimia 5.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Machi 2020.
Katika hatua nyingine, mku- rugenzi huyo alisema hali ya mfu- muko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki, Kenya kwa mwezi unao- ishia Aprili 2020 umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.62 kutoka asilimia 5.51 Machi 2020.
Alisema kwa Uganda mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Machi 2020.