27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yapasisha sheria ya marekebisho ya Katiba

MOSCOW, URUSI

MAHAKAMA ya Katiba ya Urusi imepasisha mapendekezo yaliyotolewa na Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin kwa ajili ya kurekebisha Katiba.

Taarifa iliyotolewa na Mahakama ya Katiba ya Urusi imesema kuwa, mapendekezo ya Rais Rais Putin yatakayomuwezesha kubakia madarakani baada ya kumalizika muhula wa utawala wake wa sasa hayapingani na Katiba ya nchi.

Uamuzi huo wa majaji wa Mahakama ya Katiba ya Urusi hauhitaji tena idhini ya chombo chochote cha dola.

Jumamosi iliyopita Rais Putin aliidhinisha azimio lililopasishwa na Bunge la nchi hiyo kuhusu marekebisho ya Katiba ambayo yatarefusha kipindi cha uongozi wa rais wa sasa wa nchi hiyo baada ya kupigiwa kura ya maoni ya wananchi. Kura hiyo ya maoni ya kupasisha marekebisho hayo itafanyika Aprili 22 mwaka huu.

Bunge la Urusi (Duma) Jumatano iliyopita Machi 11 lilipiga kura 383 za ndio,  pasina kura za hapana, huku wabunge 42 wakijizuia kupiga kura na kupasisha muswada wa mapendekezo ya Putin.

Baraza la Shirikisho la Urusi pia siku hiyo hiyo lilipasisha sheria hiyo inayomruhusu Putin kugombea tena urais mwaka 2024.

Uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa, aghalabu ya wananchi wa Urusi wanamuunga mkono Putin na wanamtaka aendelea kuongoza nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles