30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Mtenda jinai za kivita DRC aachiliwa huru

BRUSSELS, UBELGIJI

ALIYEKUWA kinara wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Thomas Lubanga ambaye alikuwa mtu wa kwanza kukamatwa na kufungwa jela na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), ameachiliwa huru baada ya kumaliza kifungo chake cha miaka 14.

Lubanga alipatikana na hatia ya makosa ya ukiukaji wa haki za binadamu kama mauaji na ubakaji wa raia  na kuwatumia watoto wakati akiongoza kundi la waasi la Union of Congolese Patriots (UPC) kati ya mwaka 1997 hadi 2007 katika jimbo la Ituri.

Mwezi Julai 2010, majaji waliisimamisha kesi ya Thomas Lubanga kuhusu makosa ya uhalifu wa kivita na kuamuru aachiliwe huru baada ya waendesha mashtaka kukataa kuwasilisha taarifa kwa upande wa utetezi.

Lubanga alikana mara kadhaa kutumia watoto kama wanajeshi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia mwaka 2002 hadi 2003.

Thomas Lubanga aliyekuwa kiongozi wa wanamgambo wa UPC aliongoza wanamgambo wa kabila la Hema kupigana dhidi ya watu wa kabila la Lendu.

Ghasia za kugombea ardhi ziligeuka kuwa vita vya kikabila ambapo takriban watu 50,000 waliuawa na maelfu walibaki bila makazi.

Mwezi Disemba mwaka 2015 alihamishwa kutoka gereza la ICC na kupelekwa katika gereza la Makala mjini Kinshasa kumalizia kifungo chake akiwa pamoja na mbabe mwingine wa kivita, Germain Katanga ambaye pia ICC ilimtia hatiani.

Lubanga ameachiliwa huru wakati eneo alikozaliwa la Ituri huko DRC lingali linashuhudia machafuko.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles