28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yakamilisha kusikiliza utetezi kesi mauaji ya wanafamilia 17

Malima Lubasha , Musoma

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Musoma mkoani Mara, imekamilisha kusikiliza utetezi wa washitakiwa 13 wa kesi ya mauaji yaliyotokea mwaka 2010 Mtaa wa Mgaranjabo Manispaa ya Musoma, watu 17 wa familia moja waliuawa kwa mapanga.

Kati ya washitakiwa watuhumiwa tisa wa kesi hiyo walifanikiwa kufika mahakamani mbele ya Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, Mustafa Siani na jopo la wanasheria watatu upande wa Jamuhuri wakiwakilishwa na Renatus Mkude na mawakili tisa upande wa utetezi wakiwakilishwa na Daud Mahemba.

Taswira ya utetezi kwa washtakiwa hao walioutoa kwa nyakati tofauti mahakamani hapo, walidai wao hawakufahamiana kabla, bali walikukutana magereza wakituhumiwa kuhusika na kesi ya mauaji ya watu 17 wa familia moja, utetezi ambao unakinzana na maelezo ya awali waliyotoa polisi wakati wanakamatwa.

Baada ya kusikiliza utetezi huo mahakamani hapo, Jaji Siani alipanga Desemba mosi, mwaka huu iwe siku ya kufanya majumuisho kwa wanasheria wote na baadaye kupanga tarehe ya kutoa hukumu.

Ikumbukwe watuhumiwa  tisa na wenzao wanne ambao walifariki dunia wakiwa magereza kutokana na magonjwa mbalimbali, inadaiwa Februali 16,2010 nyakati za  usiku wakiwa na silaha za jadi, ikiwemo  mapanga, sime na tochi Mtaa wa Mgaranjabo Manispaa ya Musoma walivamia nyumbani kwa  Kawawa Kinguye, kisha kuwakatakata mapanga watu 17 wa familia moja pamoja na ng’ombe wawili.

Ilielezwa  idadi kubwa ya majeruhi walifariki  eneo la tukio na katika uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi, ulionyesha mauaji hayo yalitekelezwa kama njia ya kulipiza kisasi cha mtu mmoja kuuawa kwa kosa la kuiba mbuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles