23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Nendeni mkaitumikie vema jamii -Wasira

Asha Bani -Dar es salaam

MWENYEKITI  wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Stephen Wasira amewataka wanafunzi zaidi 3,000 waliohitimu wa chuo hicho wakawe wazalendo ili kuitumikia jamii vema.

Alisema hayo mwishoni mwa wiki  alipotangaza rasmi mkusanyiko wa mahafali 15 ya wanafunzi 3,000 wa fani mbalimbali katika chuo hiko.

Aliwashauri wale wanaohitaji soko la watu waliosoma vizuri ikiwemo mafunzo ya uongozi na nidhamu kuwachukua wahitimu hao kwa kuwa watakuwa wamebobea katika eneo hilo.

“Bila kujali fani waliyosomea wote wamepewa mafunzo juu ya uongozi kwa wale ambao wanataka soko la watu waliosoma vizuri na vilevile waliosomeshwa vizuri kwa mambo ya uongozi na nidhamu basi wana nafasi nzuri ya kupata watu kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kivukoni.

” Maono ya chuo hiki ni kuandaa wasomi wa fani mbalimbali lakini vile vile kuwapa mafunzo ya uongozi na uzalendo ili waweze kuendeleza na kuongoza jamii katika maeneo mbalimbali,” alisema.

Alisema Mwalimu Nyerere  aliazimia kianzishwe kituo ambacho kitakuwa chimbuko la uongozi, 1961na kilianzishwa  N na kuita chuo cha Kivukoni shabaha yake ilikuwa kutoa mazao ya watu ambao wataongoza nchi.

Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalilo alisema wahitimu hao wamehitimu katika ngazi za astashahada, stashahada na shahada ya kwanza katika fani mbalimbali kwa wahitimu 3280 ambapo kati ya hao wanawake 1,883 sawa na asilimia 57.4 na wanaume ni 1,397 sawa na asilimia 42.5.

Alisema inaonyesha wanawake ni wengi ambao watatunikiwa vyeti vyao katika mahaali hayo

Alisema mahafali hayo ni matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa na wanafunzi hao pamoja na watumishi katika chuo hicho.

Alitaja majukumu makuu ya chuo hicho ni kutoa mafunzo katika fani mbalimbali, mafunzo ya uongozi, maadili na utawala bora pamoja na kufanya utafiti ili kupata majibu ya changamoto mbalimbali zinazokabili jamii.

Alisema chuo hicho pia kinaendesha kozi mbalimbali fupi kwa ajili ya kuwajengea uwezo watu mbalimbali  kutoka katika sekta zote za umma na binafsi ikiwepo kozi ya maadili na utawala bora pamoja na kompyuta.

Aliongeza kua mwaka huu chuo kimefanikiwa kutekeleza malengo yake ikiwemo kuongeza idadi ya udahili kwa wanafunzi kutoka Kampasi ya Kivukoni 8,43 hadi 9,54 na Kampasi ya Karume idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka wanafunzi 1,35 hadi 1,56,idadi kufikia 11,413.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles