26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA YAAMURU ALIYEFUNGWA MAISHA KWA KUBAKA AACHIWE

Na KULWA MZEE

-DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Rufaa ya Tanzania, imeamuru mrufani Said Hussein aliyefungwa maisha kwa kubaka, kuachiwa huru gerezani kutokana na makosa ya kisheria katika kufungua mashtaka.

Rufaa hiyo namba 110/2016 ilisikilizwa na kutolewa uamuzi mbele ya jopo la majaji watatu, Bernard Luanda, Batueli Mmila na Augustine Mwarija.

Hussein alishtakiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora kwa kubaka kinyume cha sheria ya kanuni namba 130 na 131 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mrufani alitiwa hatiani kwa kosa hilo na kupewa adhabu ya kifungo cha maisha jela. Aliikatia rufaa adhabu hiyo akipinga.

Katika hati ya mashtaka, mrufani alikuwa anadaiwa kuwa Februari 27 mwaka 2005, katika Kijiji cha Uchama, Nzega, alimfuata mlalamikaji shambani akiwa na panga, alimzidi nguvu, alimtishia kumuua akamwangusha na kumvua nguo za ndani kisha akambaka.

Mrufani alikuwa na sababu nne za rufaa na ya kwanza ni kwamba hati ya mashtaka ilikuwa batili kwa sababu Jamhuri walishindwa kuweka wazi kifungu gani cha sheria walitumia kumshtaki.

“Jamhuri ilikosea kumshtaki mrufani kwa kutumia sheria namba 130 na 131 bila kueleza ni kifungu gani na aya ipi katika sheria hiyo inayoonyesha kosa halisi.

“Sababu ya kwanza ya rufaa ina msingi kisheria, mahakama inaikubali, mrufani alikaa gerezani kwa miaka 12 ni kama nusu ya adhabu ya miaka 30 jela, tunarudisha suala hili kwa Mkurugenzi wa Mashtaka.

“DPP ataamua kumshtaki upya ama la, lakini akiamua kumshtaki kama atatiwa hatiani azingatie miaka 12 ambayo mrufani alikaa jela.

“Kutokana na hoja hizo, mahakama inamwondolea adhabu ya kifungo cha maisha mrufani na inaamuru mrufani aachiwe gerezani labda kama anaendelea kuwepo kwa kosa lingine,” lilisema jopo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles