22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

HASHIM RUNGWE MBARONI KWA UTAPELI

Na LEONARD MANG’OHA

-DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Chauma katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Hashim Rungwe, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa siku tano sasa akituhumiwa kutapeli zaidi ya sh milioni 70.

Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alithibitisha kushikiliwa kwa kiongozi huyo wa kisiasa na kuahidi kulitolea suala hilo ufafanuzi zaidi leo.

“Ni kweli anashikiliwa kwa utapeli wa fedha zaidi ya Sh milioni 70, lakini nimeahidi kulitolea suala hili ufafanuzi kesho (leo) kwa sababu hatuna maelezo ya kutosha kueleza sasa hivi,” alisema Mambosasa.

Alipoulizwa kuhusu nyaraka anazodaiwa kughushi kama taarifa zilivyoonekana katika mitandao ya kijamii, alisisitiza kuwa yote hayo atayatolea ufafanuzi atakapozungumza na waandishi wa habari.

Taarifa za kushikiliwa kwa Rungwe zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii jana, zikieleza kuwa anashikiliwa kwa kosa la kughushi nyaraka ambazo hata hivyo hazikuwekwa hadharani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles