23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli: Msifiche fedha zenu nje ya nchi

Anna Potinus

Watanzania wamehimizwa kuwekeza nchini na kuachana na tabia ya kukimbizia fedha zao nje ya nchi kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia wengine kufaidika na uwekezaji huo bila kujali kama waliiba fedha hizo au la.

Kauli hiyo imetolewa na Rais John Magufuli alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari Mwanakwerekwe iliyopo Mjini Magharibi na Hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Hotel Verde Azam Luxury Resort and Spa iliyopo Mtoni Unguja wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi visiwani Zanzibar.

“Viongozi ndani ya serikali zote mbili pamoja na wananchi wanaotaka kuwekeza wasiogope, ninafahamu wapo watanzania wenye fedha nyingi lakini wanaogopa kuwekeza hapa nchini badala yake wanaenda kuwekeza nje siku mkifa hizo fedha zitaliwa huko huko.

“Wenye fedha zao wawekeze hapa kwani kwa kufanya hivyo unajenga mazingira mazuri ya watu wengine kufaidika na uwekezaji wako hata kama uliiba lakini zitasaidia watanzania wengine tumeambiwa hapa wametengeneza ajira za watu zaidi ya 200 na hawa walioajiriwa kwanza wanamuombea mzee Bakhresa kwasababu wameimarika kiuchumi.

“Niwaombe sana watanzania pamoja na wanasiasa wenzangu msiogope kuwekeza, msifiche mali zenu hata kama mlizipata kiuficho mziachie wazi zikafanye kazi za watanzania, mzee Bakhresa endelea kuwafundisha watanzania wengi namna ya kuwekeza kwa manufaa ya nchi yetu,” amesema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles