27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Watuhumiwa 20 mbaroni kwa makosa ya kiuhamiaji

RAYMOND MINJA IRINGA

Idara ya Uhamiaji mkoni Iringa inawashikilia watuhumiwa 20 wa makosa ya kiuhamiaji ambao 19 ni raia wa Kenya wenye asili ya Somalia na raia 1 wa Tanzania.

Akizungumza na vyombo vya habari Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji SACI, Agnes Michael Luziga amesema watuhumiwa hao wameingia nchini kinyume na sheria ya uhamiaji Sura ya 54 Rejeo la mwaka 2016 (Immigration Act Cap 54 RE 2016)na kanuni zake.

Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa mapema wiki hii katika maeneo ya Mtera getini mkoani Iringa mara baada ya kikosi cha doria cha uhamiaji kupata taarifa za kiintelejensia kutoka kwa askari wa SUMAJKT Kituo cha mtera.

Aidha ametoa wito kwa Watanzania kuiga mfano kwa kuwafichua wahalifu wa aina hiyo kwani jukumu la  ulinzi na usalama wa taifa na mipaka yake ni la kila mtanzania.

Katika zoezi la kupambana na wahamiaji haramu Idara ya uhamiaji Tanzania inaendelea kutoa elimu kwa umma kwa njia ya televisheni, redio, magazeti, mikutano ya hadhara na mitandao ya kijamii ili kuwahasa wananchi kushiriki kwa kutoa taarifa uhamiaji pindi wanapokutanana na mtu au au kundi la watu ambao wanawatilia mashaka katika maeneo yao ya kazi ili kuwezesha idara kuchunguza na kubaini sababu za ujio wao na shughuli zao hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles