31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli atamani watendaji ‘TRA’ ya Uganda wahamishiwe Tanzania

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais John Magufuli amesema anatamani angepewa watendaji wa Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA), na wa Tanzania waende Uganda kwa mwezi mmoja tu ili awashughulikie.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ijumaa Septemba 6, jijini Dar es Salaam katika kongamano la wafanyabiashara kutoka Tanzania na nchini Uganda.
Kauli ya Rais Magufuli kuwataka watendaji hao imetokana na hatua ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kusuasua katika kuanza ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima kwenda Chongoleani mkoani Tanga.

“Leo niwape siri, nilikuwa namuuliza Rais Museveni mbona unachelewesha hili bomba, kwa sababu ya kodi ya huko ambayo umekataa kuikubali ya Dola 600 wakati utakuwa unatengeneza Dola bilioni 800 jitolee hii kodi kidogo utengeneze ajira na utakuwa unapata fedha kwa muda mrefu watu wako wa TRA wasikucheleweshe, sisi tulitaka hilo bomba liitwe Kaguta Pipeline siku tunapozindua, hao wasikucheleweshe.

“Simfundishi mzee, lakini nilipoingia madarakani nimebadilisha makamishna watano kwa miaka mitatu na nusu, si suala la kujidai lakini ni baya. Nikamwambia wewe umeng’ang’ania huyo wa kwako wa nini huko, tunatakiwa twende mbele, katika biashara kuna kupata na kukosa unatakiwa utoe ili upate zaidi.

“Kwanini ucheleweshwe na watendaji, kaka naona umekuwa mpole kabla ya wakati ule ulipopigana ulikwa mkali sasa uongeze, ongeza ukali kwenye hili.

aji, kaka naona umekuwa mpole kabla ya wakati ule ulipopigana ulikwa mkali sasa uongeze, ongeza ukali kwenye hili.

“Nimeona nilizungumze hili sitaki kuwa mnafiki, I wish (natamani) hawa watendaji wangehamia Tanzania na wa Tanzania waende Uganda nideal (nishughulike) nao kwa mwezi mmoja tu,” amesema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles