26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli alikuwa jembe langu-Kikwete

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete, amefichua kuwa siri ya kumteua Hayati Dk. John Magufuli alikuwa jembe lake na alimuamini ndio sababu akamteua katika wizara tatu tofauti.

Kikwete ameyasema hayo leo Ijumaa Machi 26, 2021 Wakati wa Ibada Maalum ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli iliyofanyika katika Uwanja wa Magufuli Chato mkoani Geita, amesema alikiwa ni mmoja wa mawaziri ambao alimuamini na kumtumaini.

Rais mstaafu wa Awamu wa Nne,, Jakaya Kikwete (kushoto) akiwa na Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania Hayati Dk. John Magufuli, enzi za uhai wake.

“Nilipokuwa Rais, Magufuli alikuwa Waziri wangu kwa miaka 10 alikuwa ni mmoja wa mawaziri niliowatumaini ndiyo maana nilimuweka kwenye wizara tatu zilizokuwa ngumu na zenye changamoto anyooshe mambo.

“Nilipoanza nilianza naye Wizara ya Ardhi nikamwambia kuwa hawa watu wa Ardhi wameshindikana wanagawa Viwanja mara nne nne wanakupa rushwa, hebu nenda pale, ukininyooshea  hiyo basi, amepigana akafikisha mahali fulani lakini mmh…hao jamaa wagumu kweli…sijui kama Rais tutapata dawa ya watu wa ardhi ukipata hiyo watu tutakupongeza…,” amesema Kikwete.

Kikwete amesema baada ya hapo alimhamishia wizara ya mifugo akiwa na lengo la kumtaka kubadilisha mfumo wa ufugaji kutoka uchungaji kuwa wa kibiashara zaidi.

“Nilitamani maziwa yawe mengi, mama iwe nzuri pamoja na ngozi, lakini nikaambiwa kuna uvuvi mwingi haramu huko baharini samki wanakwisha, ni wazi kwamba kazi ilifanyika na chamoti walikiona kwani alikuwa mpaka idadi ya sato walioko ziwa Viktoria akawa ananiambia wwe Rais ziba masikio, fumba macho.

“Baadae nilipokuwa na ajenda kubwa katika miaka mitano yangu ya mwisho maana miaka mitano ya kwanza unafanyia kuchaguliwa tena na miaka mitano ya mwisho unafanyia legacy(ukiacha alama), watu wakukumbuke kwa kitu haji.

“Namimi nilikuwa nataka watu wanikumbuke kwa kuunganisha Barabara za lami, nikasema kwamba jembe langu huyu basi nakupeleka wizara ya ujenzi nakuhakikishia tutakaa hapa kwa miaka mitano sikusudii kukubadili lakini tukubaline kwanza Barabara za kufanyia kazi, akasema wewe mzee niwezeshe tu mengine niachie, na nikweli nimestaafu kama kuna mko hatujaubgajisha ni Kigoma na Katavi pia Arusha na Mara,” amesema Kikwete.

Aidha, amesema kuwa katika kipindi jicho cha kufanya naye kazi kwa Katibu ndipo alipojiridhiaha kuwa Magufuli anaouwezo wa kubebela dhamana kubwa hata ya kuliongoza Taifa.

“Kwani alikuwa mchapakazi lakini alikuwa havumilii uzembe, wizi wala ubadhirifu, alipojitokeza kuomba uteuzi wa kuwa mgombea urais ndani ya CCM 2015sikusita kumpendekeza katika majina matano niliyoyafikisha kwenye kikao cha juu cha Chama jina la Magufuli lilikuwa la kwanza,” amesema Kikwete.

Amesema kuwa walikubaliana na wajumbe kupitisha majina matano bila kiongeza wala kupunguza ndipo wakapiga kura na kupata majina matatu likiwemo la Hayati John Magufuli.

“Kwa hiyo waswahili wanasema akutukanayw hakuchagulii tusi, kwa hiyo unaposikia minong’ono kuwa JK hampendi Magufuli hee…nyiemMie au JK mwingine.

“Ooh JK anachukua JPM unamchukiaje mtu ambaye ulimkabizi ilani ya Chama, Mimi na yeye tulikuwa tukutane Machi, alipokuwa ziarani mkoani Dar es Salaam anikabidhi nyumba aliyonijengea,” amesema Kikwete.

Kikwete amekiri kuwa kifo cha Hayati Magufuli ni pigo kubwa kwa familia na Taifa kwa ujumla.

Mwili wa Hayati Dk. John Magufuli unatarajiwa kupumzishwa jioni hii katika makaburi ya familia yaliko nyumbani kwake Chato mkoani Geita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles