27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli afagia Ma-DC 78

RAIS Dk. John Magufuli
RAIS Dk. John Magufuli

*  Wateule wa Kikwete watoswa rasmi

*  Amtumbua bila ganzi Magesa Mulongo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli  ameshusha presha  iliyokuwa imepanda kwa wakuu wa wilaya huku kila mmoja  akisubiri hatima yake, kwa kufanya uteuzi   jana.

Amewateua wakuu wa wilaya 139 na kufanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa.

Taarifa iliyotolewa Ikulu Dar es Salaam jana  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ilisema pia  amewateua wakurugenzi watendaji wa halmashauri 22 kuwa wakuu wa wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.

Katika mabadiliko hayo, sura mpya za vijana zimefanikiwa kuingia huku kundi kubwa la wakuu wa wilaya wa Serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa na  Rais mstaafu Jakaya Kikwete, wakijikuta wakiangukia pua.

Balozi Kjazi alisema,  Rais    ametengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Dk. Charles Mlingwa.

Vilevile, amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Zainab Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Zainab anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango ambaye uteuzi wake ulitenguliwa miezi kadhaa iliyopita.

Mwingine aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa ni  aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) katika Serikali ya awamu ya nne, Dk. Binilith Mahenge ambaye anakwenda  Mkoa wa Ruvuma.

Dk. Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu  aliyehamishiwa katika Ofisi ya Waziri Mkuu   ambako atapangiwa majukumu mengine.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, alisema katika uteuzi huo Rais Magufuli, amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri kwa kuwapumzisha wale mbao umri wao ni zaidi ya miaka 60.

Rais Magufuli amewashukuru walioachwa kwa utumishi wao mzuri akisema kuwa pale ambako itahitajika, Serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.

Katika mabadiliko hayo, wakuu wa wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39.

Balozi Kijazi alisema   wakuu wa wilaya 78   wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.

Orodha kamili ya walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya na wilaya zao katika mabano ni kama ifuatavyo:

ARUSHA

Mrisho Gambo (Arusha), Alexander Mnyeti (Arumeru)       , Rashid Taka (Ngorongoro),   Daniel Chongolo (Longido), Idd Kimanta (Monduli),  huku aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Therezia Mahongo (Karatu).

DAR ES SALAAM

Ally Hapi (Kinondoni),  Sophia Mjema (Ilala), Felix Lyaviva (Temeke), Hashim Mgandilwa (Kigamboni) na Hamphrey Polepole (Ubungo).

DODOMA

Vumilia Nyamoga (Chamwino), Christina Mndeme (Dodoma), Simon Odunga (Chemba), Sezeria Makutta

(Kondoa), Elizabeth Simon      (Bahi), Jabir Shekimweli (Mpwapwa),         John Palingo (Kongwa).

GEITA

Josephat Maganga (Bukombe), Martha Mkupasi (Mbogwe), Hamim Gwiyama (Nyang’wale),      Herman Kipufi (Geita),  Shaaban Ntarambe (Chato).

IRINGA

Jamhuri William (Mufindi), Asia Abdallah      (Kilolo) na Richard Kasesela (Iringa).

KAGERA

Saada Mallunde (Biharamulo), Geofrey Ayoub (Karagwe), Richard Ruyango (Muleba), Col. Shaban Lissu (Kyerwa), Deodatus  Kinawilo (Bukoba),      Lt. Col. Michael Mtenjele (Ngara) na     Lt. Col Denis Mwila    (Missenyi).

KATAVI

Aliyekuwa kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka 2015, Rachiel Kasanda (Mlele), Lilian Matinga,       (Mpanda), Saleh Mhando (Tanganyika).

KIGOMA

Samsoni Anga (Kigoma), Col. Martin Elia Mkisi (Kasulu), Col. Hosea Ndagala (Kakonko), Mwanamvua Mlindoko (Uvinza), Col. Elisha Gagisti (Buhigwe) na Luis Peter Bura (Kibondo).

KILIMANJARO

Onesmo Buswelu (Siha), Kippi Warioba (Moshi), Aaron Mmbago (Mwanga), Fatma Toufiq (Rombo), Gelasius Byakanwa (Hai), Rosemary Senyamule (Same).

 LINDI

Rukia Akhibu Muwango (Nachingwea), Joseph Mkirikiti

(Ruangwa), Sarah  Chiwamba (Liwale), Shaibu Ndemanga (Lindi) na Christopher Ngubiagai (Kilwa).        –

MANYARA

Raymond Mushi (Babati), Chelestion Mofungu (Mbulu), Sara Ally   (Hanang’), Tumaini Magessa (Kiteto), Zephania Chaula (Simanjiro).

MARA

Simon Chacha (Rorya), Emile Ntakamulenga (Serengeti      ), Lydia Bupilipili (Bunda), Anarose Nyamubi (Butiama), Glodious Luoga (Tarime),       Dk. Vicent Naano (Musoma).

MBEYA

Rehema Madusa (Chunya), Claudia Kitta (Kyela), William Paul (Mbeya), Chalya Nyangidu (Rungwe),    Reuben Mfune (Mbarali).

MOROGORO

Siriel Shaid Mchembe (Gairo), James Ihunyo (Kilombero),  Mohamed Utali (Mvomero), Regina Chonjo (Morogoro),      Kassema Joseph (Ulanga),       Adam Mgoyi

(Kilosa), Majula Mateko Kasika (Malinyi).

MTWARA

Aziza Mangosongo (Newala), Joakim Wangabo (Nanyumbu),    Dk. Khatibu Kazungu (Mtwara), Seleman Mzee (Masasi), Sebastian Walyuba (Tandahimba).

MWANZA

Dk. Leonald Massale (Ilemela), Mtemi Simeon (Kwimba), Emmanuel Kipole (Sengerema), Mary Onesmo

(Nyamagana), Hadija Nyembo (Magu), Estomihn Chang’ah (Ukerewe) na Juma Sweda (Misungwi).

NJOMBE

Ruth Msafiri (Njombe), Andrea Tsere

(Ludewa), Ally Kassige (Wanging’ombe) na Veronica Kessy (Makete).

PWANI

Majid Mwanga (Bagamoyo), Filberto Sanga (Mkuranga), Juma Njwayo       (Rufiji), Shaibu Nunduma (Mafia), Asumpter Mshama (Kibaha), Happyness William (Kisarawe), Gulamu Kifu (Kibiti).

RUKWA

Dk. Khalfan Haule (Sumbawanga), Said Mtanda

(Nkasi), Julieth Binyura (Kalambo).

RUVUMA

Luckness Amlima (Namtumbo), Cosmas Nshenye (Mbinga), Isabera Chilumba (Nyasa), Juma Homela (Tunduru) na Polet Mgema    (Songea).

SHINYANGA

Nyambonga  Taraba (Kishapu), Fadhili Nkulu (Kahama), Josephine Matiro (Shinyanga).

SIMIYU

Tano Mwera (Busega), Sefu Shekalaghe (Maswa), Festo Kiswaga (Bariadi),       Joseph Chilongani (Meatu),   Benson Kilangi (Itilima).

SINGIDA

Jackson Masako (Mkalama), Mwembe Geofrey (Manyoni), Elias Tarimo (Singida), Fikiri Said

(Ikungi),   Emmanuel Luhahula (Iramba).

SONGWE

Samwel Jeremiah (Songwe),  Joseph Mkude (Ileje)

Ally Maswanya (Mbozi)    na Juma Irando (Momba).

TABORA

Geofrey Ngudula (Nzega),  Busalama Yeji (Kaliua),  Mwaipopo Gabriel (Igunga), Peres Magiri (Sikonge), Queen Mlozi (Tabora),  Angelina Kwingwa (Urambo),   Wakili Gabriel Simon Mnyele (Uyui)

TANGA

Thobias Mwilapwa (Tanga), Mwanaisha Tumbo (Muheza),  Yona Maki (Mkinga), Zainab Issa (Pangani), Godwin Gondwe (Handeni),  Robert Gabriel (Korogwe),

Sauda Mtondoo (Kilindi) na Januari Lugangika (Lushoto).

Katibu Mkuu Kiongozi alisema wakuu wapya wa mikoa  wataapishwa Ikulu Dar es Salaam keshokutwa   na baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.

Vilevile, wakuu wote wa wilaya walioteuliwa nao wametakiwa kufika Ikulu Dar es Salaam keshokutwa    kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi   na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles