21.4 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Magu yakaribisha wawekezaji kutumia hekari 3,000

Na Sheila Katikula, Mwanza

Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza imetenga eneo la ya hekari 3,000 kwenye kijiji cha Matela kilichopo kata ya Nyanguge kwa ajili wawekezaji ili kuongeza kasi ya maendeleo ya sekta ya viwanda, kilimo na biashara wilayani humo.

Hayo yameelezwa Agosti 16, 2021 na Mkuu wa Wilaya hiyo, Salim Kali wakati wa uzinduzi wa chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi cha Pine College kilichopo kijiji cha Kisesa ‘A’ kata ya Bujora na kusisitiza kuwa wilaya yake ina ardhi ya kutosha kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.

Amesema wamejipanga katika kila idara kukabili vishoka wa masuala ya aridhi na hakuna atakayekwamisha ama kuchelewesha, maendeleo pindi mwekezaji atakapohitaji eneo na serikali inasimamia na kulinda  rasilimali za taifa na mali za Watanzania.

Aidha, Kali alimpongeza mwekezaji kwa kujenga chuo kwenye eneo hilo kwani hakukuwa na huduma kwani  kitachagiza kutoa fursa na ajira za kudumu sanjari na kuongeza pato la serikali kwa kulipa kodi.

“Chuo hiki kitatoa kozi mbalimbali kwa wanafunzi, kitasaidia  watu kupata kazi, Jeshi la akiba pia wapo mafunzoni pindi watakapo hitaji kombati tutawaleta hapa watushonee, hatuwezi kupeleka mbali wakati  chuo kipo hapa kwetu,” alisema Kali.

Mkurugenzi wa Chuo cha Pine College, Blaze Ndege alisema kabla ya kuanzisha chuo hicho waliangalia uhitaji wa jamii na wamekusudia kutoa elimu mbadala kwa watu wa waliohitimu kidato cha nne, chuo na waliomaliza darasa la saba ili waweze kupata ujuzi mbadala.

Alisema  chuo hicho kitatoa  kozi tano ikiwemo ufundi umeme wa majumbani ushonaji, mapambo, urembo, masomo ya kompyuta na wanatarajia kuongeza kozi nyingine.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa eneo kilipo chuo hicho, Lucas Magembe alisema atahakikisha anaweka ulinzi na usalama kwenye chuo hicho ili kulinda mali za mwekezaji na kuweka mazingira salama ya kujifunzia.

Mwananchi wa eneo hilo Ryoba Masubo alisema ujio wa chuo hicho ni fursa kwa wananchi kwa sababu ya kitachagiza maendeleo na fursa kwa jamii inayozunguka chuo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles