32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Magonjwa ya presha, saratani tishio Dar

dsc_9743
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Grace Magembe.

NA HADIA KHAMIS-DAR ES SALAAM

MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na mikoa jirani waliopimwa afya kupitia kampeni ya ‘Afya Cheki’ wamegundulika kuwa na shinikizo la damu, moyo na saratani ya shingo ya kizazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Grace Magembe, alisema wananchi waliojitokeza katika kampeni hiyo wengi wamegundulika kuwa na maradhi yasiyokuwa ya kuambukiza.

Alisema maradhi hayo hayapewi kipaumbele na ndio maradhi yanayoongoza kwa idadi kubwa ya vifo hivi sasa.

“Kupitia kampeni ya ‘Afya Cheki’ wananchi wengi waliopimwa wamegundulika kuwa na maradhi yasiyokuwa ya kuambukizwa kama vile shinikizo la damu, figo, saratani ya shingo ya kizazi pamoja na tezi dume,” alisema.

Alisema kwa siku moja zaidi ya wananchi 12,500 walijiandikisha kwa ajili ya kuonwa na madaktari bingwa kati yao 9,100 wameonwa na kupatiwa huduma za afya.

Alisema huduma ya afya cheki itaendelea kutolewa katika hospitali zote za serikali hivyo wananchi waendelee kuwa na utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara.

Akizungumza wakati wa kufunga kampeni hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema kwa kutambua umuhimu wa afya za wananchi wa Mkoa wake atahakikisha elimu inawafikia wananchi wengi katika wilaya zao.

Alisema idadi kubwa ya watu katika kampeni hiyo imetokana na huduma ya bure inayotolewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles