23.5 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Magari 821 yakamatwa kwa makosa 943 Morogoro

Na Ashura Kazinja, Morogoro

JESHI la polisi mkoani Morogoro limeendelea na oparesheni ya kuzuia ajali za barabarani kwa kukamata jumla ya magari 821 na makosa 943  ikiwemo makosa ya mwendokasi, ubovu wa magari, ulevi, kutokuwa na leseni.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilim, amesema oparesheni hiyo inayofanyika katika barabara zote za mkoa wa Morogoro, zinalenga kuzuia makosa yanayofanyika barabarani ambayo yamekuwa ni chanzo cha ajali zinazotokea.

Musilimu amesema oparesheni hiyo iliyofanyika Aprili 4 na 5, mwaka huu katika kizuizi cha Mikese kuanzia saa 6 hadi 9 usiku, inafanyika ili kudhibiti mwendokasi, kukamata madereva wanaopita magari maeneo yaliyokatazwa (overtake), kutozingatia alama na michoro ya barabarani, ubovu wa magari na ulevi wa madereva na makosa mengine.

Akiyachambua makosa hayo 943 amesema makosa ya mwendokasi ni 130, ubovu wa magari 110, kutozingatia ratiba makosa 70, kuzidisha abiria makosa 58, kutokuwa na RATRA makosa 35, kutokuwa na bima 42, kutokufunga mikanda 38, kuendesha kwa njia ya hatari makosa 47, kutokuwa na leseni makosa 17 huku makosa mengine yakiwa ni 273.

“Tumekamata magari 13 ambayo yanabeba abiria bila kibali cha LATRA, bila leseni za madereva na bila magari hayo kukaguliwa na jeshi la polisi kwa mujibu wa taratibu, magari hayo yamesafiri usiku na kwa kuendeshwa kwa mwendokasi, kuovateki ovyo na kuwa chanzo cha ajali, magari hayo yanasafiri kwenda Mbeya, Tunduma, Bukoba, Kahama na maeneo mengine” anasema Kamanda Musilimu.

Wakati huo huo Kamanda Musilim amesema madereva 22 wa pikipiki na bajaji wamefikishwa mahakamani huku wengine wakiandikiwa faini kwa jumla ya makosa 124, ambayo ameyataja kuwa ni kutovaa kofia ngumu makosa 100, kutokuwa na bima 11, kutokuwa na leseni 6  pamoja na kubeba abiria zaidi ya mmoja maarufu kama mishikaki watano.

Hata hivyo Kamanda Musilim ametoa wito kwa wananchi kuacha kupanda magari usiku, na badala yake watumie usafiri wa mabasi yaliyopo, na kuwataka wamiliki wa mabasi nchini kufuata taratibu zilizowekwa ili kulinda maisha ya watu, na kwamba oparesheni hiyo ni endelevu hivyo taratibu zifuatwe ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles