24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mafuta ya petroli, dizeli bei juu

kaguo+titusGRACE SHITUNDU NA TUNU NASSOR,
DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya itakayoanza kutumika leo ambapo mafuta ya petroli na dizeli yamepanda huku mafuta ya taa yakishuka.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo, alisema bei ya jumla na rejareja ya mafuta aina zote imebadilika ikilinganishwa na bei elekezi iliyotolewa Aprili, mwaka huu.
Alisema bei ya rejareja kwa mafuta ya petroli imeongezeka kwa Sh 111 kwa lita sawa na asilimia 6.32 huku dizeli ikiongezeka kwa Sh 23 kwa lita sawa na asilimia 1.37.
“Kuanzia leo lita moja ya petroli itauzwa kwa shilingi 1,866 kwa Jiji la Dar es Salaam na shilingi 2,097 kwa mikoa ya pembezoni ikiwamo Kigoma ambapo bei ya zamani ilikuwa ni shilingi 1,755 Dar es Salaam na shilingi 1,986 kwa Mkoa wa Kigoma,” alisema Kaguo.
Alisema mafuta ya dizeli yatauzwa kwa Sh 1,695 Dar es Salaam na Sh 1,938 kwa mikoani ambapo bei ya awali ilikuwa ni Sh 1,672.
Kaguo alisema mafuta ya taa yameshuka kwa Sh 31 kwa lita sawa na asilimia 1.86 ambapo yatauzwa kwa Sh 1,624 Dar es Salaam na Sh 1, 867 kwa mikoani.
Akifafanua zaidi, Kaguo alisema bei ya jumla ya kwa petroli ni Sh 1,761.05, dizeli Sh 1,589.58 na mafuta ya taa Sh 1,518.86.
Alisema mabadiliko hayo yametokana na kupanda kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia pamoja na kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani.
“Wananchi wategemee mafuta kupanda zaidi ifikapo Julai, mwaka huu kwani madhara ya kupanda kwa dola ya Marekani na kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania yataonekana,” alisema Kaguo.
Akizungumza suala la uhaba wa mafuta katika baadhi ya vituo vya mafuta nchini, alisema inatokana na kushindwa kupakiwa kwa wakati.
Alisema tangu Mei Mosi mwaka huu kulikuwa na mfululizo wa mapumziko ambayo yalikumbana na Jumatatu ya mgomo wa madereva wa mabasi na malori ambayo ndiyo wasafirishaji wa mafuta ndani na nje ya nchi.
“Mapumziko ya Mei Mosi na mgomo vimechangia kwa kiasi kikubwa katika suala hili la uhaba wa mafuta katika baadhi ya vituo na endapo yatapakiwa leo ina maana watu wa mikoani watapata mafuta kuanzia siku nne zijazo,” alisema Kaguo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles