26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Escrow yakwamisha miradi

Na Jonas Mushi, Dar es Salaam
SAKATA la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, limechangia kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya mwaka 2014/15.
Hatua hiyo imesababisha hadi kufikia Machi mwaka huu, ni asilimia 38 tu ya miradi ndiyo iliyotekelezwa.
Hayo yalibainishwa jana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dk. Philip Mpango, wakati akihojiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.
Kamati hiyo iliitaka Tume ya Mipango kutoa sababu za kutotekelezeka kwa miradi huku bajeti ya mwaka unaomalizika ikiacha deni la Sh trilioni nne ambazo hazikupelekwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Akijibu hoja hiyo, Dk. Mpango alisema changamoto kubwa ilikuwa ni kutopatikana kwa fedha zilizokuwa zimepangwa ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa zinategemea wahisani ambao waligoma kutoa fedha kwa sababu ya sakata la Escrow.
“Sakata la Escrow lilisababisha wahisani kuwa na mtazamo hasi kwa Serikali yetu ambapo walitoa masharti ambayo baada ya Serikali kuanza kushughulikia suala hilo wapo walioleta fedha, lakini wengine bado wameendelea kugoma kuleta fedha kutokana na sakata hilo.
“Naweza kusema Serikali imekuwa na ugumu wa kupunguza mihemko ya kutaka kufanya mambo mengi yanayohitaji fedha, huku ikiwa haina vyanzo vya uhakika vya kupata fedha hizo,” alisema Dk. Mpango.
Aidha alisema kwa sasa tume imekuja na mpango wa kuhakikisha miradi iliyoanza inamalizika kabla ya kuanza miradi mipya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles