25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mafuta ya petroli bei juu

SERIKALI imependekeza kuongeza tozo ya mafuta ya petrol na dizeli kutoka Sh 50 kwa lita hadi Sh 100 kwa lita, ikiwa ni ongezeko la Sh 50 kwa lita.
Akizungumzia kuhusu ongezeko hilo wakati akiwasilisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/16 bungeni mjini Dodoma jana, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, alisema mafuta ya taa yanapaa kutoka Sh 50 kwa lita hadi Sh 150 kwa lita, ikiwa ni ongezeko la shilingi 100 kwa lita ili kuondoa uwezekano wa kuchakachua.
“Hatua ya kuongeza tozo ya mafuta ya petroli inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh milioni 139,786.8. Fedha hizi zote zitaelekezwa katika Mfuko wa Umeme Vijijini (REA) kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za usambazaji wa umeme vijijini,” alisema.
Alitoa pendekezo la kupewa mamlaka ya kusamehe tozo ya mafuta ya petroli kwenye miradi inayotekelezwa kwa misaada ya wafadhili na yenye mikataba isiyohusisha utozaji wa tozo hiyo.
Alipendekeza mafuta ya dizeli kupanda kutoka Sh 263 kwa lita hadi Sh 313 kwa lita, ikiwa ni ongezeko la Sh 50 kwa lita.
Aidha alisema: “Hatua ya kuongeza ushuru wa barabara inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh milioni 136,370.2. Napendekeza kuwa, fedha zitakazopatikana kutokana na ongezeko hilo la ushuru wa barabara zitumike katika kugharamia usambazaji wa umeme vijijini kupitia mfuko wa REA.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles