30.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mafuriko yatikisa tena China

Beijing, China

WATU zaidi ya milioni 1.76 wameathiriwa na mafuriko yaliyotokea katika Jimbo la Shanxi lililoko Kaskazini mwa China.

Majanga hayo yanajitokeza ikiwa ni miezi isiyozidi mitatu imepita tangu mvua kubwa iliposababisha vifo vya watu zaidi ya 300 katika Jimbo la Henan.

Mafuriko ya safari hii yametokana na mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita na kusababisha uharibifu wa nyumba katika wilaya na miji zaidi ya 70.

Kwa mujibu wa vyanzo vya mamlaka katika mahojiano na Shirika la Habari la Xinhua, nyumba 17,000 zimeharibika, hali hiyo ikisababisha watu zaidi ya 120,000 kuyakimbia makazi yao.

Aidha, athari hizo zimeambatana na vifo vya maafisa wa polisi wanne, kwa mujibu wa kile kilichoripotiwa na Xinhua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles