Na Mwandishi Wetu
Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kali maeneo ya kusini na magharibi mwa Irani yameua takriban watu 23 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa, kwa mujibu wa vyombo vya habari.
Awali, Wizara ya Mambo ya Ndani iliwashauri watu wa Irani kuahirisha safari zao lakini pia kufuata onyo lilitolewa kwa uzito na Shirika la Usimamizi wa Maafa ambalo lilitoa ujumbe wa maandishi ili kuwaonya watu kuhusu kutumia njia ambazo zinaweza kukabiliana na mafuriko, ikiwa ni tahadhari pia kwa wale waishio katika milima na mabonde ya mto.
Janga hili limetokea kipindi hiki wakati wa Mwaka Mpya wa Irani, Nowruz, pia ni likizo, ,uda ambao Waislamu wengi wanasafiri nchini.
Kulikuwa na mvua nzito za dakika 15 ambazo zilisababisha mafuriko kuenea katika jiji hilo lakini pia yasemekana idadi ya majeruhi ingekuwa chini endapo wtu wngefuata tahadhari iliyotolewa kabla ya mafuriko.