26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

UMOJA WA ULAYA WASITISHA OPERESHENI OKOA WAHAMIAJI MEDITERANIA

Umoja wa Ulaya umesitisha kupeleka manowari katika operesheni yake ya kukabiliana na wahamiaji haramu katika bahari ya Mediterania maarufu kama operesheni Sophia kufuatia kutokuwepo kwa makubaliano baina ya mataifa wanachama.

Hata hivyo chanzo kimoja kutoka Umoja wa Ulaya kimeliambia shirika la habari la Ujerumani DPA kwamba operesheni hiyo itaendelea kuhudumu kwa njia ya anga na kutoa mafunzo kwa walinzi wa pwani wa Libya.

Mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wamepewa muda wa hadi leo mchana kuwasilisha pingamizi la kutokukubaliana na uamuzi huo, vinginevyo utatekelezwa kwa miezi sita. Wasiwasi umeendelea kutawala kwa miezi kadhaa iwapo operesheni hiyo inaweza kuendelea kufuatia mzozo mkubwa wa wahamiaji.

Mwezi Disemba, operesheni Sophia iliongezewa muda wa miezi mitatu hadi Machi 31 kama suluhu ya mpito baada ya mataifa wanachama kushindwa kusaini makubaliano ya kuchukua majukumu ya muda mrefu ya kupokea wahamiaji ikiwa ni pamoja na Italia yenye misimamo mikali dhidi ya wahamiaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles