24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Solskjaer kukabidhiwa timu wiki hii

MANCHESTER, ENGLAND

UONGOZI wa klabu ya Manchester United, umepanga kumalizana na kocha wao wa muda, Ole Gunnar Solskjaer, kwa kumpa mkataba wa kudumu kabla ya kumalizika wiki hii.

Viongozi wa timu hiyo walikutana Jumatatu wiki hii kwa ajili ya kujadili suala hilo, hivyo kwa mujibu wa Dailymail, kuna uwezekano mkubwa wa kocha huyo kupewa mkataba wa moja kwa moja wiki hii.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46, tangu ameichukua timu hiyo kama kocha wa muda Desemba mwaka jana, hadi sasa ameisimamia kwa michezo 19 ya michuano mbalimbali na kufanikiwa kushinda michezo 14.

Solskjaer alipewa nafasi hiyo ya kuwa kocha wa muda baada ya uongozi kumfukuza kocha mkuu, Jose Mourinho, kutokana na mwenendo mbaya wa timu, lakini tangu achukue nafasi ya kocha huyo, timu imekuwa na mafanikio makubwa ya kushinda michezo mbalimbali.

Kutokana na uwezo anaouonesha kocha huyo, wadau mbalimbali na mashabiki wa klabu hiyo walitoa maoni yao wakiwataka viongozi kuhakikisha wanampa mkataba wa kudumu kabla ya kumalizika ule wa miezi sita aliopewa.

Kiungo wa Manchester United, Nemanja Matic, amefunguka na kusema, wakati umefika wa kocha huyo kuachiwa timu moja kwa moja, huku wachezaji wengine wakidai kufurahia uhusiano wao na kocha huyo.

“Kila mmoja anaamini kuwa Solskjaer ni kocha bora, kwa upande wangu nitakuwa na furaha kubwa akipewa mkataba wa kudumu, ninaamini viongozi watafanya hivyo. Hata hivyo, lazima tuwape sifa na wale wasaidizi wake, Mike Phelan, Michael Carrick na Kieran McKenna,” alisema mchezaji huyo.

Manchester United kwa sasa inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, ikiwa na pointi 58 baada ya kucheza michezo 30, inapigania kuingia katika nafasi nne za juu. Jumamosi wiki hii United itakuwa kwenye uwanja wa nyumbani kupambana na Watford.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles