26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mafunzo kazini yatengeneza ajira 50 NMB

Na Mwandishi Wetu

Benki ya NMB imefanikiwa kutengeneza fursa za ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu zaidi ya 50 kupitia programu yake maalumu ya mafunzo ya vitendo kazini iliyoanzishwa takribani miaka 10 iliyopita.

Mbali na kutoa fursa kwa wahitimu wasio na kazi na sifa zinazohitajika kuajiriwa moja kwa moja, uwekezaji huo umeiwezesha NMB kuzalisha wafanyakazi wenye ujuzi na weledi mkubwa katika maswala ya kifedha na kibenki.

Wahitimu watano wa program ya mafunzo ya uongozi ya Benki ya NMB wakiwa katika hafla ya maafali ya kumaliza mafunzo iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika Makao makuu ya Benki ya NMB. Wahitimu hao walitunuliwa vyeti baada ya kufanya mafunzo ya miaka miwili 2018 – 2020 na kuajiriwa moja kwa moja na benki hiyo.

Akizungumza wakati wa mahafali ya wahitimu watano wa mwaka huu wa programu hiyo, Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema mchakato huo si muhimu tu kwa benki hiyo na washiriki wake bali pia kwa tasnia ya fedha na nchi kwa ujumla.

Mahafali hayo yalifanyika ijumaa iliyopita makao makuu ya NMB jijini Dar es Salaam na tayari zoezi la kupata wanafunzi wengine 10 watakaoanza mafunzo hayo mapema mwakani yanayochukua miaka miwili limekamilika.

Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Benki ya NMB, Margareth Ikongo akimvalisha kofia mmoja wa wahitimu katika Program ya mafunzo ya uongozi ya Mwaka 2018-20202 ya benki ya NMB (NMB Management Training). Kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi.

“Kama benki inayoongoza kwa faida nchini, tunalo lengo lakutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana hususani kwenye masuala ya ajira nchini, hivyo vijana hawa tuliwachukua walivyomaliza kozi mbalimbali vyuoni na kuwapa ujuzi katika maeneo ya kazi ili waweze kuwa na uzoefu wanapoajiriwa,” alifafanua Mponzi.

Kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, Mponzi aliwataka wahitimu hao kuitendea haki imani ya benki hiyo kwao na kuwa wafanyakazi bora na waadirifu. Pia aliwaomba kuitumia nafasi hiyo adimu waliyopata kuisogeza NMB mbali zaidi kimafanikio na kuisaidia kuendelea kutoa huduma bora.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB, Margaret Ikongo, aliyewapongeza wahitimu kwa kuzishinda changamoto walizokumbana nazo baada ya masomo vyuoni. Kiongozi huyo alisema hiyo ni mojawapo ya sababu zilizochangia utendaji wao bora na ufanisi kazini mpaka kuajiriwa moja kwa moja na NMB.

“Jinsi mlivyofanya kazi kwa bidii, uvumilivu, juhudi, maarifa, nidhamu na kujituma kipindi cha mafunzo ya  miaka miwili, naomba msiishie hapa tu, bali muende mkalete mapinduzi kwenye kila kazi mnayogusa ili benki yetu iendelee kusonga mbele,” alisema Ikongo wakati wa mahafali hayo yaliyoambatana na kutunukiwa vyeti.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, akimvalisha nembo ya NMB mmoja wa wahitimu wa Program ya mafunzo ya uongozi mwaka 2018-2020. kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya NMB, Margareth Ikongo.

Akizungumza kwa niaba ya wahitimu wenzake, Agnes Nyanzala, alikiri kuyafurahia mafunzo ya vitendo kwa miaka miwili, yaliyojaa uwezeshaji uliowapa urahisi wa kiutendaji, kiasi cha kuivutia NMB na kuwapa ajira.

Nyanzala alisema kuwa kwa sasa wameiva vya kutosha na wana ari kubwa katika kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi na kwamba wako tayari kwa mamapambano ya kunyanyua ustawi wa NMB kuanzia mwaka ujao wa 2021.

Programu ya mafunzo kazini ya NMB ilianzishwa mwaka 2009 na kila baada ya miaka miwili benki hiyo uwatuma wataalamu wake wa raslimali watu kwenda vyouni kutafuta wanafunzi wenye vipaji wapate mafunzo ya vitendo ndani ya benki.

Lengo lake kuu ni kuendeleza bomba ya talanta ya watu wenye ujuzi kwa maeneo ya msingi ya biashara ndani ya benki na kuunda fursa kwa wahitimu wasio na kazi na sifa zinazohitajika ili kuendeleza ustadi katika mazingira ya kibenki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles