DAMASCUS, Syria
IMERIPOTIWA kuwa hadi sasa asilimia 92 ya wananchi raia wa Syria wameshakombolewa kutoka mikononi mwa maeneo yanayoshikiliwa na wapiganaji wa kikundi cha kigaidi cha Kiislamu nchini humo, ISIS.
Kwa mujibu wa jarida linalochapishwa kila wiki na Wizara ya Ulinzi ya Urusi, Krasnaya Zvezda, raia hao wameokolewa kutokana na msaada wa jeshi hilo tangu serikali ilipoamua kujitosa katika mgogoro huo.
Jarida hilo lilieleza kuwa katika vita hiyo vikosi vya anga vya Urusi vilifanya kazi kubwa ya kupambana na wapigaji hao wapatao 517. Lilieleza kwamba katika mapambano hayo vilifanikiwa kuharibu zaidi ya vituo 1,260 vilivyokuwa vikimilikiwa na kundi hilo la kigaidi la kimataifa.
Lilieleza pia kwamba idadi hiyo inajumuisha zaidi vituo 139 vya kurushia makombora na vingine 129 ambavyo vilikuwa vikitumika kuwahifadhi wapiganaji wa kundi hilo.