ADAM MKWEPU Na MITANDAO,
WAMESHITUKA usajili wa mbuzi kwenye gunia! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya klabu ya soka ya Real Madrid kujiweka pembeni katika mbio za kusaka saini ya kiungo mkabaji kinda wa timu ya Juventus, Paul Pogba.
Mabingwa hao wa Ulaya, kwa sasa hawana mpango wa kumsajili nyota huyo wa Juventus, na badala yake mbio hizo kuhisusia klabu ya Manchester United.
Uamuzi huo wa Madrid kususia usajili wa Pogba uliamuliwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu iliyopita.
Inadaiwa kwamba dau alilohitaji nyota huyo limeathiri uamuzi wa klabu hiyo kutaka kumsajili.
Kutokana na uamuzi huo huenda Pogba hasisaini klabu hiyo kwa kipindi hiki cha usajili ingawa si asilimia 100 uamuzi huo unaweza kufanya kazi.
Kwa sasa nyota huyo yupo katika mipango ya Manchester United ambao wanapambana ili kupata huduma ya kiungo huyo wa Juventus.
Kwa sasa Pogba yupo tayari kuzungumza na kocha mpya wa Manchester United Jose Mourinho ili kurudi katika klabu hiyo inayotumia uwanja wa Old Trafford.
Baada ya kuona kuna uwezekano wa kutua katika klabu hiyo amethibitisha kwa kusema kwamba United ni zaidi ya familia yake.
Hata hivyo maisha yake ya baadae yapo katika klabu ya Juventus ambao wanamchukulia kama asset itakayofanya klabu hiyo kupata mkwanja mkubwa.
Pogba akiwa nchini Marekani kwa ajili ya mapumziko anasema kwamba tayari alikwisha zungumza na Mourinho ili kuweka mambo sawa.
Tayari wakala wake Mino Raiola ameshafanya biashara kubwa na United kwa kusajili wachezaji wawili wakiwa mikononi mwake, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan.
Mwingine, Romelu Lukaku, ambaye yupo chini ya Raiola,yupo mbioni kujiunga na hotspot 1Oak.
Kwa mujibu wa website ya Sky Sport inasema kwamba ni muda mrefu tangu klabu ya Madrid kuwa katika mipango ya kumsajili kinda huyo kutokana na ubora wake ndani ya uwanja na kuonekana kama angewagharimu Euro milioni 250.
Pia inaeleza kwamba kiwango cha fedha cha mchezaji huyo akiwezi kuwa zaidi ya Euro milioni 100 ambayo tayari klabu ya Manchester United imetajiwa ili kupata saini ya mchezaji huyo.
Kwa upande wa Radio Marca ilidai kwamba wiki chache zilizopita Juventus ilihitaji Madrid kulipa Euro milioni 120 pamoja na Ton Kroos kuwa sehemu ya biashara hiyo na ilionekana kama dili hilo linaweza kufanyika.
Pamoja na hayo, mshahara wa nyota huyo uliterajiwa kwa mwaka kuwa Euro milioni 14 ili kuhama Turin.
Hivyo kutokana na utaratibu wa malipo ya kodi ya nchini Hispani nyota huyo angetakiwa kulipwa jumla ya Euro milioni 130 kwa misimitano.
Kama haitoshi, wakala wa nyota huyo Raiola alitarajia kupata asilimia 20 au 30 ya fedha hizo, inategemea na kiasi kitakacholipwa.
Matumizi yote hayo, yanafanya mchezaji huyo kulipwa jumla ya Euro milioni 250 ambayo ni nyingi ukilinganisha na uwezo wake uwanjani.
Kama Madrid watakubali kumlipa nyota huyo Euro milioni 14 kwa mwaka atakuwa mchezaji wa pili kulipwa fedha nyingi katika klabu hiyo baada ya Cristiano Ronaldo.
Hivyo ataweza kumzidi, Sergio Ramos, Gareth Bale na Karim Benzema, kitu ambacho kinaweza kuwa na athari kubwa ndani ya klabu hiyo na vyumba vya kubadilisha nguo.
Bado Madrid wanahitaji kumbakisha Alvaro Morata Bernabeu kwa kuwa hawaoni umuhimu wa kumfanya kama nyenzo ya kubadilishana na Pogba.
Kutokana na hali hiyo, Madrid haioneshi kuwa tayari kwa kumsajili mchezaji huyo huku wakijua wazi kwamba ujio wake unaweza kuvuruga kikosio kizima cha timu hiyo.
Kingine kinacho wakatisha tama Pogba hakuwa katika kiwango kizuri katika michuano ya Euro 2016.
Kucheza kwa kiwango cha chini katika michuano hiyo inaweza ikawa si sababu ya msingi lakini mchezaji huyo hana cga ziada ambacho wachezaji wa timu hiyo hawana.
Kwa kuwa ili kuweza kutoa fedha nyingi ni lazima mchezaji mwenywe aoneshe kitu cha ziada alichonacho lakini si kwa Pogba.
Madrid inajivunia kusheheni wachezaji wazuri eneo la kati zaidi ya Pogba akiwamo, Toni Kroos, Luka Modric, James Rodriguez, Isco, Casemiro na Mateo Kovacic.
Azina hiyo ya kutosha ya wachezaji wa akiba wenye uwezo zaidi ya  Pogba au wenye kulingana na mchezaji huyo huenda ndio sababu ya jeuri ya Madrid katika kubadili uamuzi wake.
Kovacic, Casemiro, Lucas Vasquez, si maarufu kibiashara ya usajili ilivyo sasa lakini kwa Galactico ndio usajili muhimu uliochangia kutwa Ubingwa wa Ulaya msimu uliopita.
Pogba ni kiungo ambaye katika soka la wachezaji msimu huu yupo juu kutokana na kipaji alichonacho kwani anaweza kufunga, kutoa mchango wa bao na kuwa miongoni mwa wachezaji wanao toa hamasa kwa klabu kubwa.
Hata hivyo si vema kutegemea maajabu makubwa kutoka katika miguu yake kwa kuwa bado ana mengi ya kujifunza kama mchezaji chipukizi.
Zaidi ni kwamba, Pogba ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa lakini kwa aina ya wachezaji wa Madrid bado nafasi yake ndogo katika kikosi cha timu hiyo.