29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Madonna anazeeka na ubora wake

Bridgestone Super Bowl XLVI Halftime ShowNA ADAM MKWEPU

KUNA wakati ambao matukio katika maisha huendana na umri wa mhusika ili kueleweka katika jamii bila kuangalia shughuli au kazi anayofanya.

Wakati huo ukifika ndipo jamii inaweza kutenganisha kati ya kijana na mzee katika uwajibikaji na uchangiaji wa maendeleo.

Nchi ya Marekani imeonekana kuwa tofauti na wakati ili kutofautisha mambo anayoweza kufanya kijana na mzee kutokana na mazingira yaliyokuwapo nchini humo.

Utofauti huo umeathiri hata katika tasnia ya muziki na uigizaji. Safu hii tunaangalia nyota mkongwe wa muziki wa pop duniani raia wa Marekani, Madonna Louise Ciccone, ambaye alifanya vituko jukwaani alipokuwa anawarusha watu wakila starehe nchini Australia.

Nyota huyo anayekadiriwa kuwa na utajiri wa zaidi milioni 700 amejikuta akiwa kwenye ‘front page’ kwenye mitandao mbalimbali duniani hususani ile ya Australia ambako alikuwa akifanya tamasha eneo la Rebel Heart.

Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 57, alikuwa kwenye gumzo hilo baada ya kumvua sidiria makusudi shabiki wake wa miaka 17, Josephine Georgiou, huku akidai kuwa ni muda wa msichana huyo kula bata na kufurahia maisha.

Madonna akiendelea kutumbuiza kwenye tamasha hilo, alimwita msichana huyo ili apande jukwaani na baada ya kufanya hivyo  ndipo alipoamua kumvua sidiria.

Hata hivyo, mwanamitindo huyo hakuonesha kuchukizwa na kitendo hicho badala yake akadai kwamba halikuwa jambo la ajabu kwake huku akionekana mwenye kutabasamu muda wote.

Tabasamu hilo alionesha hata alipohojiwa na vyombo vya habari  vya nchi hiyo badala yake aliendelea kumtetea Madonna kwa kudai kwamba watu wanajaribu kumtengenezea mazingira ya kuonekana kwamba si mtu mzuri kwenye jamii.

Msichana huyo anadai kwamba hakukuwa na kitu chochote kibaya kilichofanywa na Madonna licha ya kumvua sidiria na kubaki kifua wazi mbele ya mashabiki zaidi ya 1,000.

Georgiou anasema kwamba yeye ndiye anayetakiwa kuona kitendo hicho ni udhalilishaji na anashangazwa na watu wanaojaribu kumzungumzia.

Zaidi ni kwamba msichana huyo alipatwa na mshangao baada ya kujikuta akiwa pembeni mwa Madonna, alidai kuwa mwanamuziki huyo ndiye anayevutiwa naye.

“Nilimwona Madonna akiniangalia na kutabasamu kama vile alikuwa akiniambia kitu, alafu akawa anazungumza na wavulana upande mwingine wa jukwaa kisha wote wakawa wananitazama.

“Waliniangalia kama walikuwa wakinizungumza jambo na baada ya dakika 10, Madonna aliniuliza kama napenda kucheza muziki,” anasema Georgiou.

Msichana huyo alifanikiwa kutua kwenye ukumbi huo baada ya kulipia tiketi ya dola 99 baada ya zile zilizokuwa zikiuzwa dola 500 kumalizika.

Alifanikiwa kuingia ndani ya ukumbi baada ya Madonna akiwa tayari kamaliza kuimba wimbo wa kwanza kabla ya kuanza wa pili ndipo alipopata nafasi ya kuitwa jukwaani.

Georgious anadai kwamba wakati akiwa anathibitisha uhalali wa tiketi yake alikutana na wavulana ambao walimtaka baadaye kupanda jukwaani.

Pia msichana huyo anadai aliambiwa kabla angepanda jukwaani ili kuimba na kucheza pamoja na Madonna, alikubali na kuona bahati kukutana na mwanamuziki aliyekuwa akimpenda na kumhusudu kwa miaka mingi.

“Sioni kama kuna jambo lolote la udhalilishaji kwangu nahisi hakukutokea kitu chochote ingawa siku ya pili niliamka nikakuta simu yangu imevunjika hata hivyo sikujali,” anasema.

Mrembo huyo alipohojiwa na polisi alikiri kwamba Madonna alimwambia angemwita jukwaani na baada ya kupanda mwanamama huyo aliamwambia kuwa anavutiwa naye.

Mama wa msichana huyo, amedai kwamba mwanamuziki Madonna, hakutambua kwamba mrembo huyo alikuwa na umri wa miaka 17 kutokana na umbo kubwa alilokuwa nalo.

Pia anaongeza kuwa mwanawe ana furaha na tukio hilo kwa kuwa halijamfanya kuchanganyikiwa kama watu wanavyodai.

Hata hivyo, polisi wa Quensland, Australia, wanadai kuchunguza ukweli wa jambo hilo kama kuna malalamiko yoyote dhidi ya mwanamuziki huyo.

Tabia ya Madonna kila siku imekuwa ikionekana kujaa vituko hasa akiwa kwenye ziara zake baada ya kudaiwa kuwa na  ugomvi na aliyekuwa mumewe wa zamani, Guy Ritchie, juu ya mtoto wao, Rocco (15).

Baada ya tukio hilo, mashabiki walionekana wakiwa na hasira  kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakimwita Madonna ‘asiyejali’.

Pia mashabiki hao walichukizwa na tabia ya mwanamuziki huyo kuchelewa kwenye tamasha hilo huku waandaaji wakionekana kusikitika kwa kupungua mapato siku hiyo.

Kwa mujibu wa jarida la Quays la nchini Australia, Madonna alilazimika kulipa faini kwa kuchelewa Desemba mwaka jana alipotakiwa kufanya tamasha kwenye Jiji la Manchester, England.

Mwaka 2008, Madonna alilipa faini ya pauni 135,000 sawa na dola 258,326 kwa kuchelewa tamasha lililofanyika uwanja wa  Wembley England.

Hata hivyo, mwanamuziki huyo alikuwa akifanya tamasha lake nchini Australia kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 23 ambapo ameahidi kufanyia filamu tamasha atakalofanya uwanja wa Olympic Park uliopo Sydney nchini Australia mwishoni mwa wiki.

Nyota huyo atakuwa amebakiwa na matamasha mawili ya mwisho baada ya miezi saba akiwa katika mpango huo ambao umemfanya kutembea nchi mbalimbali duniani.

Nyota huyo hasiyeishiwa vituko muda mrefu amekuwa akipanda jukwaani na wachekeshaji, waigizaji na mashabiki wake hata hivyo mwisho wa wiki hii anatarajia kuchagua mashabiki wake wachache ili kupanda nao jukwaani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles