CHAMA cha Muziki wa Disco nchini (TDMA) kinatarajia kuadhimisha siku ya DJ duniani ambayo huadhimishwa Machi 9 ya kila mwaka.
Katibu Mkuu wa TDMA, Asanterabbi Mtaki, ilisema kwa kuanzia, maadhimisho hayo kwa Tanzania yatafanyika jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kutoa mchango wa ma DJ kwa jamii.
Alisema maadhimisho hayo yatawakutanisha ma DJ wa vituo vya redio, klabu, baa, disko, hip hop, reggae, road show na ma DJ wengine wote nchini.
“Maandalizi ya maadhimisho hayo yanaendelea kufanyika vizuri na tunaziomba ofisi za ma DJ kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kufanikisha tukio hilo,” alisema Mtaki.
Maadhimisho hayo yatafanyika katika mikoa mbalimbali ambapo mikoa iliyothibitisha kufanya ni Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya.