25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MADIWANI WADAI FEDHA ZAO ZILIZOANZISHA KAMPUNI YA NYAMA BADALA YA MACHINJIO

Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam wametaka Sh bilioni 1.5 zilizochangwa na Halmashauri za Ilala, Temeke na Kinondoni kwa ajili ya kuanzisha machinjio ya kisasa zirejeshwe katika halmashauri hizo kwa kuwa hakuna machinjio iliyoanzishwa hadi sasa.

Kati ya fedha hizo kila halmashauri ilichanga Sh milioni 500.

Wakizungumza leo Jumanne Januari 23, katika kikao cha madiwani, wamesema fedha zilichangwa lakini machinjio haikuanzishwa badala yake ilianzishwa kampuni ya nyama ambayo nayo haikufanya kazi.

Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge (CCM), amesema hata hisa za kampuni hiyo ziko kwenye majina ya watu binafsi waliokuwa watumishi wa Jiji la Dar es Salaam.

“Waliochukua fedha hizi wapo tujadiliane tujue tunafanyaje, lakini sisi Kinondoni tunataka Sh milioni 500 zetu tulizochanga,” amesema Mnyonge.

Kutokana na hali hiyo, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, amesema kwenye bajeti ya sasa fedha hizo hazikutengwa hivyo akaagiza suala hilo likajadiliwe kwanza kwenye kamati halafu liletwe kwenye baraza kwa hatua zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles