27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani Sikonge watakiwa kutatua kero za wananchi

Na Allan Vicent, Sikonge

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora wametakiwa kuhakikisha kero za wananchi zinatatuliwa katika kata zao na kusimamia vyema mikakati ya kimaendeleo inayowasilishwa katika vikao vya halmashauri hiyo.

Rai hiyo imetolewa leo, Desemba 15, na Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Rashid Magope ambaye ni diwani wa kata ya Tutuo (CCM) alipokuwa akitoa neno la shukrani katika kikao hicho ambapo wajumbe wote 28 walimpigia  kura za ndiyo.

Amesema kuwa Halmashauri hiyo imepata mafanikio makubwa sana katika miaka mitano iliyopo kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya madiwani, watendaji na watalaamu, hivyo akasisitiza umuhimu wa kudumishwa kwa mshikamano huo.

‘Tunalo deni kubwa kwa wananchi, Sikonge ya leo sio ya jana imebadilika sana, naomba kila mmoja akasimame kwenye zamu yake, akawatumikie wananchi ipasavyo, akasikilize kero zao na kuzitafutia ufumbuzi’, amesema Magope.

Magope amesisitiza kuwa ndoto yake ni kuona halmashauri hiyo ikiendelea kupanda hadhi na kuwa na Mamlaka ya Mji ili kuharakisha maendeleo ya wananchi ikiwemo kuboresha mandhari ya Mji huo.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Sikonge, Joseph Kakunda amesema kuwa hatma ya udiwani na ubunge wao katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025 iko mikononi mwao, hivyo wanapaswa kutumia nafasi hiyo vizuri kwa kuchapa kazi kwa bidii ili wapiga kura waendelee kuwaamini.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mayeka Mbussa (diwani wa kata ya Kilumbi) amesema wako tayari kuwatumikia wananchi kwa viwango vya juu ili Chama Cha Mapinduzi kiendelee kuaminika kwa wananchi.

Wakitoa salamu za chama katika kikao Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani humo, Anna Chambala, Katibu wake, Magdalena Ndwete na Mwenezi Bakari Malugu waliwapongeza wakazi wa wilaya hiyo kwa kuchagua madiwani wote wa chama hicho, na kuahidi kuwa chama kitaendelea kuwatumikia kwa viwango vya juu.

Wamesema kuwa uchaguzi umeisha hivyo wakawataka mbunge na madiwani wote kusimamia utekelezaji ilani ya uchaguzi ya chama kwa vitendo ikiwemo kutatua kero za wananchi na kutekeleza ahadi zao kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles