24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Madereva walevi wanavyokatisha maisha ya Watanzania

Polisi wakichunguza ajali
Polisi wakichunguza ajali

NA MWANDISHI WETU,

KANDA ya Kaskazini inatajwa kuwa na ajali nyingi zitokanazo na madereva walevi, jambo ambalo linasababisha ulemavu kwa watu wasio na hatia sambamba na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

Hali hii imekuwa ikitokana na madereva kuwa na tabia ya unywaji pombe usio wa kistaarabu, yote haya yanasababishwa na kukosa elimu juu ya masuala ya unywaji pombe.

Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2013 ajali za barabarani kwa Mkoa wa Kilimanjaro  zilikuwa 697 ikilinganishwa na ajali za mwaka 2014 ambapo zilikuwa 332; ikiwa ni punguzo la ajali 365 sawa na asilimia 52, Kwa Mkoa wa Arusha, takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2013  ajali zilikuwa 563 kwa kipindi cha Januari hadi June na kwa mwaka 2014 ajali zilikuwa 164 ambazo ni punguzo la ajali ni 399 sawa na asilimia 71.

Takwimu hizi zinaonyesha jitihada kubwa zilizofanyika kupunguza ajali za barabarani zitokanazo na ulevi ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Kwa sababu hiyo, Oktoba 18 na 20 mwaka huu, Kampuni ya Bia ya Serengeti ilizindua kampeni inayohamasisha matumizi sahihi ya pombe au unywaji pombe kistaarabu.

Kampeni hii ni hatua muhimu katika sekta ya biashara ya pombe kwa kutambua changamoto inazokabiliana nazo hususan katika masuala ya uwajibikaji kwa jamii.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkuu wa Usalama wa Barabarani mkoani Arusha, Mhandisi Nuru Kacharia anasema kulishirikisha Jeshi la Polisi, kikosi cha usalama barabarani, kunaonyesha ni kwa jinsi gani SBL wanatilia maanani suala zima la usalama barabarani hasa kwa kuzingatia matokeo ya ulevi na uendeshaji wa vyombo vya moto.

Kamanda Kacharia anasema uzoefu unaonyesha kwamba watu wengi hujisahau na kujiingiza katika ulevi wa kupindukia bila kuzingatia vyombo vya moto wanavyoendesha.

“Ni jambo lilisilopingika kuwa uzembe na unywaji wa pombe kupita kiasi vina athari kubwa kwa jamii. Madhara hayo hayamuathiri mtumiaji wa pombe pekee, bali uhatarisha maisha na kuathiri mustakabali wa watu wengi,” anasema Kamanda Kacharia na kufafanua kuwa “Kwa mantinki hiyo, ni janga la jamii nzima huduma zetu za afya zimeelemewa kwa kiasi kikubwa na wale waliojeruhiwa katika masuala yanayohusiana na ajali na uhalifu; taasisi zetu za masuala ya sheria zimeelemewa vilivyo; uzalishaji unaathirika mno na kwa mlolongo huo, ukuaji wa pato la taifa hubakia kuwa wa kiwango cha chini.”

Akielezea jinsi kampeni hii itakavyosaidia kutokomeza ajali za barabarani, anasema; “ama kwa hakika, sote kwa ujumla wetu tunaathirika na sote tunalo jukumu la kuchangia namna bora ya kukabiliana na tatizo la ulevi. Nafurahi kuona kwamba wazalishaji wenyewe wa vinywaji vya pombe wametambua kuwa biashara wanayofanya kwa wateja wao inahitaji uwajibikaji na umakini wakati wa kutumia.”

Kwa upande wake Mkuu wa Usalama Barabarani mkoani Kilimanjaro, Kamanda Zauda  Mohammed, anasema kwa mkoa wake makosa ya ulevi ni mengi ambapo kwa kipindi cga Januari hadi Juni 2015 kulikuwa na makosa 279 sawa na asilimia 65 na kwa mwaka huu kuanzia Januari hadi Juni 2016 makosa yalikuwa 148 ambayo ni sawa na asilimia 35.

Kamanda Zauda anasema makosa hayo yamepungua na kuahidi kuwa kwa kushirikiana na wadau hasa SBL watahakikisha wanatoa elimu kwa madereva ili kudhibiti ongezeko la ajali zitokanazo na ulevi.

Katika hatua nyingine, SBL  ilizindua kampeni hiyo mkoani Kilimanjaro Oktoba 18 mwaka huu, ili kuhamasisha matumizi sahihi ya unywaji pombe.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkaguzi Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Peter Mizambwa, anasema kulishirikisha jeshi la polisi, kikosi cha usalama barabarani, kunaonyesha ni kwa jinsi gani SBL wanatilia maanani suala zima la usalama barabarani hasa matokeo ya ulevi na uendeshaji vyombo vya moto.

“Kwa mantiki hiyo, ni janga la jamii nzima huduma zetu za afya zimeelemewa kwa kiasi kikubwa na wale waliojeruhiwa katika masuala yanayohusiana na ajali na uhalifu; taasisi zetu za masuala ya sheria zimeelemewa vilivyo; uzalishaji unaathirika mno na kwa mlolongo huo, ukuaji wa pato la taifa hubakia kuwa wa kiwango cha chini.”

Mizambwa anasema anafurahi kuona kwamba wazalishaji wenyewe wa vinywaji vya pombe wametambua kuwa biashara wanayofanya kwa wateja wao inahitaji uwajibikaji na umakini wakati wa kutumia.”

Anasema kuwa kampeni hiyo ya unywaji wa kistaarabu inakusudia kuwafikia vijana wengi pamoja na watu wa rika la juu kwa kuwataka kuelewa hatari ya matumizi ya pombe na kufanya uamuzi ambao utanusuru maisha yao.

Naye Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha, anasema kampeni ya unywaji pombe kistaarabu inalenga kuwapa walengwa elimu kwamba mtumiaji wa pombe hahitaji kutawaliwa na pombe na kuipa nafasi ibadili mustakabali wa maisha yake.

Anasema vifo na ajali nyingi hutokana na uzembe au ulevi wa watu ambao si waathirika wakubwa wa pombe, ambao wangeweza kuwa waangalifu kama wangechukua tahadhari na kujifikiria mara mbili au kama marafiki zao wasingewahamasisha kuongeza moja au mbili,” anahitimisha Hawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles