30.2 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mabondia Champion wa Kitaa waahidi burudani kesho

NA WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

MABONDIA watakaopanda ulingoni kesho katika nusu fainali ya kumsaka Champion wa Kitaa, wameahidi kutoa burudani kwa mashabiki wa masumbwi kwenye ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam.

Wanamasumbwi hao kila mmoja ametamba kuibuka kinara wakati wa kupima uzito leo Februari 19,2022 kwenye Uwanja wa Zakhiemu.

Kati ya mapambano 10 yanatarajia kupigwa, huku pambano kubwa likimkutanisha Hamad Furahisha dhidi ya Maganga Kulwa.

Mabondia Shaban Kaoneka(Kushoto) na Ramadhani Adam (kulia) wakitambulishwa na kocha wa mchezo huo Super D baada ya kupima uzito leo.

Akizungumzia mchezo huo, Maganga ametamba kuwa anapanda ulingoni akifahamu ana kazi maalumu ambayo ametumwa na mashabiki wake wa ndondi hivyo hatawaangusha.

“Mimi nimetumwa kazi sitaki masihala, wanangu wa Zakhiem wananijua, nawaomba muje muone kazi ya Championi wa Kitaa ndiyo mimi hapa,” ametamba Maganga.

Naye Furahisha amesema atamuonesha kazi mpinzani wake kwa sababu shoo haikuwa yake, ameingilia kati.

Kwa upande wake Shabani Kaoneka anayezichapa na Ramadhani Adam, ameahidi kurudi ulingoni kwa kishindo baada ya awali kutangaza kustaafu mchezo huo.

“Watu wangu wa Mbagala najua ‘mmenimiss’ sana, ndugu yenu nimerudi,mimi nilikuwepo nilitangaza kustaafu sawa lakini nimeona bado umri unaruhusu. Mimi vita ya ngumi naijua, kesho mapema tu namaliza kazi,” amejinadi Kaoneka.

Aidha Mratibu wa mapambano hayo Bakari Khatibu kutoka Peaktime Media, amesema maandalizi yamekamilika, kiingilio ni sh 3000 na kuwataka mashabiki wa ngumi kujitokeza kwa wingi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles