24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania watakiwa kuchangamkia fursa kilimo cha Vanilla

NA WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

WATANZANIA hasa vijana wametakiwa kuchangamkia fursa ya kilimo cha Vanilla kutokana na zao hilo kuwa na uhitaji mkubwa duniani na bei yake ipo juu kuliko bidhaa nyingine.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Vanilla International Ltd, Simon Mukondya wakati akitoa elimu kwa wakazi wa Dar es Salaam leo Februari 20,2022 katika mafunzo yaliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regence.

Amesema huu ni wakati wa kuchangamkia fursa hiyo ambapo tayari tayari baadhi ya Watanzania wameanza kuwekeza katika kilimo hicho chenye fedha nyingi.

“Tunawahamasisha sana wakulima hasa vijana kila mtu anayependa kulima na kujifunza, tunatoa elimu bure kuhusu kilimo hiki. Zao la vanilla lina umuhimu hasa katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ikiwamo vinywaji.

Mkurugenzi huyo amewataka watanzania kuondoa wasiwasi katika kuwekeza kwenye kilimo hicho kwani wametoa fursa ya kuwasaidia wakulima hadi atakapovuna mazao yake.

“Vanilla International Ltd, imetengeneza kijiji cha wakulima wa vanilla mkoani Njombe ambapo Mtanzania anayehitaji kuwekeza tunampatia shamba kulingana na kiasi cha fedha anachohitaji kuwekeza na kumtunzia mazao yake.

“Pia kama una eneo lako popote sisi tuna uwezo wa kukusaidia kufanikisha kilimo hicho kwa kukulimia na kutoa elimu jinsi ya kuitunza Vanilla,” amesema.

Amefafanua kuwa gharama za kuwekeza katika kijiji cha Vannila kilichopo Njombe ambacho wanakimiliki ni kuanzia sh. milioni tano na kuendelea.

Ameeleza kuwa unapowekeza milioni tano kwa mwaka una uwezo wa kupata kipacho cha zaidi ya milioni 20 na ni zao endelevu linalodumu kwa miaka mingi shambani ambapo mtu anaendelea kuvuna kila mwaka.
Amesema kuwa vanilla ni zao lenye fedha nyingi ambapo kilo moja inafikia milioni moja za Kitanzania.
“Uzuri ni kwamba mkulima anayewekeza kwetu, sisi ndiyo tutakuwa wanunuzi wa mazao yake lakini akitaka kuuza sehemu nyingine pia tunamruhusu,” amefafanua Mukondya.

Ameeleza kuwa kwa sasa wawekezaji waliowekeza katika mashamba yao wanafikia zaidi ya 240 tangu walipoanza na mazao yao yanaendelea vizuri shambani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles